SHETANI ANASILIMU NA KUMTAPISHA UCHAWI MGONJWA BAADA YA KUSOMEWA RUQYAH

Assalaamu alaykum
Leo nimeona niwafafanulie wasomaji wangu mambo machache kuhusu mashetani (mapepo) kwani watu wengi wamekuwa na uelewa mdogo kuhusu viumbe hawa.

Ukweli ni kwamba majini ni viumbe miongoni mwa viumbe wa mwenyezimungu kama Qur'aan inavyotueleza
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ 
"sikuumba majini na watu illa waniabudu" Adhariayaati:56

hapo tunapata ushahidi kuwa majini na wanaadamu wameumbwa na Allaah kwa ajili ya ...ibada tu.

na baada ya kuasi majini na wanaadamu ndio wakaitwa mashetani lakini maarufu kwa jina hilo la mashetani ni majini.
pia ni vyema tukatambua kuw awapo majini wema kama walivyokuwepo wanaadamu wema na pia wapo majini waovu mfano wa wanaadamu vilevile.

itambulike kuwa wapo majini waislamu,wakristo tena walokole, mayahudi,pia wapo wanaojitambulisha kwa makabila mbalimbali
nimepata kumlingania jinni wa kilokole na nilimtambua baada ya kupanda kichwani kwa mgonjwa nia kuanza kunikemea kama wafanyavyo walokole,

Hii ilikuwa mwaka 2010 nilifuatwa na mmoja wa majirani zangu na kunishitakia tatizo la binti yake aliyekuwa anashindwa kwenda shule kwa sababu ya mashetani wakati huo akiwa kidato ch nne!

siku ya kwanza nilipoelezwa matatizo ya binti huyo ilikuwa alhamisi sikumbuki tarehe lakini ilikuwa mwezi april,niliishia kuyasomea maji kisomo cha Ruqyah kisha nikawaaga na kuondoka kwakuwa nilikuwa na haraka.

nyuma yangu kumbe kulitokea matatizo mazito kiasi cha ksababisha mgonjwa kufungwa mikono na miguu niliyafahamu haya baada ya kurudi siku ya pili baada ya swala ya ijumaa,

siku hiyo wakachukua namba zangu za simu lipofika saa 11:30 jioni wakanipigia simu kuwa hali ni mbaya kwakuwa sikuwa mbali na kwao nikarudi na kumkuta mgonjwa hana fahamu.

Nikaanza kumsomea kisomo cha Ruqyah ya muda shetani akapanda nikamlingania kuachana na dhulma alidai hana dini nikamlingania juu ya uislamu akanielewa ALHAMDU LILLAAH akasilimu na akaondoka, mara akapanda mwingine wa kike akaanza kufanya dhihaka mbalimbali lakini kwa kuwa nina fahamu vitimbi vyao sikujali nilipoendelea na kisomo akaanza vituko vyake akiniambia ushindwe katika jina la yesu nami nikamuambia utashindwa wewe katika jina la ALLAAH.

Ilinichukua muda mrefu wa kisomo ndipo kibao kilipombadilikia na kuanza majuto akimtaja yesu kwamba amemdanganya! nikamwambia sio kweli nikamueleza ukweli aliokuja nao yesu na jinsi ulivyopindishwa!

Kumbe aliwahi kuwa muislamu akadanganywa na sheatani mkristo akartadi,kwakuwa yule mgonjwa alikuwa akilalamikia maumivu ya kifua nilimuamuru yule shetani autoe uchawi wake akasema atakuja kuutoa mumewe (shetani wa kiume)kwani ndiye aliye uweka.
nikamlimngania uislamu akaukubali LILLAHIL HAMDU na yeye akasilimu,muda wa swala ya maghribi ulikuwa umeshafika tukaenda kuswali,

Tuliporudi nikaanza kusome dua kwa ajili ya kumuomba ALLAH alikinge eneo husika baada ya kuondoa picha zote za viumbe ahai ndani.
kabla sijamaliza kusoma dua shetani akapanda kwa mgonjwa na kisomo kiliendelea kwa muda mrefu sana mwisho ALLAAH kaleta tawfiq yake kwani shetani alisalimu amri akakubali kuutoa uchawi aliomlisha mgonjwa na nilipomuhoji alimlisha wakati gani akasema wakati alipokuwa anakula chipsi shuleni (siku aliyoanguka)

Pia alilinganiwa uislam akasilimu na kutoka baada ya muda mfuoi mgonjwa akarejewa na fahamu zake, nilipomuuliza mimi ni nani aknitaja jina langu na pia aliwatambua ndugu na wazazi wake,
nilipomuuliza kuhusu maumivu aliyokuwa anayalalamikia akajibu kuwa hayasikii tena! ALHAMDU LILLAAH kwani mung ndie aliyeyatenda yote mimi nilikuwa ni sababu tu.

Jumatatu yule binti akaanza kwenda shule kama kawaida,
Hawa mungu alitaka kuwaokoa na shirki kwani walishakwenda kwa mganga na kutakiwa kuku saba na mbuzi wawili,

INSHAA ALLAAH TUTAENDELEA KUELEZA MENGINE YALIYOMKUTA BINTI HUYU KUTOKA KWA MASHETANI KATIKA WAKATI MWINGINE NI MIMI NDUGU YAKO UST.HEMEDI I.PALIKE
KWA MASWALI,USHAURI NA KAMA UNAHITAJI KUSOMEWA DUA PIGA SIMU NAMBA +255715604488,-+255752604488 Na +255774604488

NB:sina nia ya kuwakejeli watu kwa imani yao, kwani baadae inshaa ALLAH nitawaeleza pia kuhusu majini waislamu niliopata kuwalingania kwa wagonjwa na vituko vyao.