Sifa njema ni za Mwenyezimungu Mlezi wa viumbe wote, Na Rehma na amani zimwendee Mtume Muhammad S.A.W ambaye ALLAH amemtuma ili awe ni Rehma kwa viumbe wote. Pia ziwaendee Aali na Maswahaba wake wote na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya malipo.
Assalaamu alaykum,
Kwanza kabisa nichukue fursa hii kuwaombea kwa Allah afya njema wagonjwa na wasomaji wangu wote kutoka sehemu mbalimbali duniani, kama vile HOLAND,CANADA,SAUDIA,OMAN na hapa nyumbani TANZANIA, ambao wamekuwa wakiwasiliana nami huku wakitaka kujua mambo mbalimbali kuhusu elimu hii ya tiba sahihi hakika wamekuwa wakinipa moyo kwa kujua kuwa wapo watu wanaofuatilia ninayowaelekeza na wengine wakinielezea zile faraja wanzopata mara watumiapo taratibu ninazowapa.leo nakusudia kuwaelezea athari ya Qur'aan dhidi ya uchawi na mashetani.
Ndugu Msomaji tunaomba mchango wako ili utuwezeshe kutoa kitabu cha dua za tiba na kinga ambacho kimesheheni shuhuda na mawaidha mbalimbali ni kitabu kitakachowasaidia, kuwaelimisha watu wengi zaidi, Toa sadaka yako sasa na wewe uingie katika watakaopata thawabu za watakaoongoka kutoka katika ushirikina na maovu mbalimbali, gharama za uchapaji wa kitabu ni kubwa hivyo msaada wako ni muhimu tuchangie kwa njia zifuatazo:-
TIGO PESA No. 0715604488 M-PESA No. 0758293138
kwa wale wasomaji wetu wa nje ya nchi wawasiliane nami kwa simu na whatsapp namba +255715604488
Ndugu Msomaji tunaomba mchango wako ili utuwezeshe kutoa kitabu cha dua za tiba na kinga ambacho kimesheheni shuhuda na mawaidha mbalimbali ni kitabu kitakachowasaidia, kuwaelimisha watu wengi zaidi, Toa sadaka yako sasa na wewe uingie katika watakaopata thawabu za watakaoongoka kutoka katika ushirikina na maovu mbalimbali, gharama za uchapaji wa kitabu ni kubwa hivyo msaada wako ni muhimu tuchangie kwa njia zifuatazo:-
TIGO PESA No. 0715604488 M-PESA No. 0758293138
kwa wale wasomaji wetu wa nje ya nchi wawasiliane nami kwa simu na whatsapp namba +255715604488
ATHARI YA QUR'AN DHIDI YA UCHAWI NA MASHETANI
Ndugu msomaji Qur'an ni maneno ya Allah yenye miujiza na athari mbalimbali ndani yake nami nimekuwa nikishuhudia miujiza na athari hizo mara kwa mara katika kazi zangu za kila siku.
Miongoni mwa miujiza hiyo nimepata kumsomea mama mmoja aliekuwa akisumbuliwa na shetani aliyekuwa akimtaka awe mganga wakati nilipomaliza kumsomea yule mama ananiuliza Ustadh umemuona mtu aliyenisimamia hapa? nikamjibu hapana , akaniambia kuwa amesimamiwa na mtu akiwa tumbo wazi huku mwili wake ukiwa umekoboka {umebabuka} kuanzia usoni mpaka kitovuni, na akilalamika kitendo ninachomfanyia si kizuri.
Naam ujumbe wa Qur'aan ulikuwa umefika mahala pake na hapo inathibitika kuwa Shetani huunguzwa na kuteswa sana na Qur'aan.
Na baada ya siku chache yule mama taabu zote zilizokuwa zikmsumbua katika mwili wake zilimwisha na Alhamdu LILLAH aliendelea vyema sikupata kusikia tatizo lolote kutoka kwake, hakika ALLAH ana fadhila kubwa.
Mfano mwingine ni wa siku za hizi karibuni kuna dada mmoja amekuwa akitokewa na wadudu na wanyama na watu mbalimbali wakimtisha na kumfanya awe na mashaka muda mwote hasa akiwa nyumbani kwake, baada ya kuniletea taarifa hii nikampangia siku ya kwenda kumsomea nyumbani kwake ili kwa uwezo wa Allaah tuwafukuze mashetani.
Na mara baada ya kufika siku hiyo nikaondoka mimi na wenzangu watatu tuafanya kisomo kwa kila mtu kusimama katika ukuta wake kisha tukayasomea maji kisomo kingine na kuyamwaga maji hayo kwenye pembe za nyumba na baada ya siku mbili yule dada akaja ofisini na kunieleza kuwa alimuona mtu aliyekuwa akimtisha akiwa anakimbia huku akionekana kuchanganyikiwa na hali ile aya kuwaona viumbe wenye kumtisha haikumtokea tena nizi pia ni katika fadhila na rehma za ALLAH yapo mengi lakini Inshaa ALLAH nitakuwa nikiwaelezea kila nikipata nafasi. Wassalaamu alaykum.
Pia unaweza kunitafuta kwa namba zangu hapo juu ukihitaji kutoa au kupokea ushauri. ama ukiwa na shida yoyote kwa sasa napatikana Magomeni Kagera, D'Salaam