DUA KWA AJILI YA KUONDOSHA MATATIZO NA DHIKI MBALIMBALI- Sehemu ya 1

Msomaji wangu mpendwa,
Assalaam alaykum

Sifa njema ni za Allaah ambaye ndiye alieumba mbingu na ardhi na vilivyomo katika siku sita na wala kazi hiyo haikumchosha hata kidogo, ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa na hafanani na chochote wala yeyote, Na ziada ya Rehma na amani zimfikie Mtume wetu Muhammadi Swalla llaahu alayhi wasallam ambaye ameletwa ili awe ni rehma kwa viumbe wote, na rehma na amani ziwafikie Aali zake na Maswahaba zake na watakaowafuata mpaka siku ya malipo.

Leo ni vizuri tukaingia katika somo lihusulo dua kwa ajili kuondosha dhiki na matatizo mbalimbali kama zilivyoelekezwa na Mtume S.a.w.
Na ni vizuri tukajua kwamba tukimuomba  Allaah atuondolee jambo linalotusumbua au atupe tunalolihitaji
kuna faida nyinginezo tunazozipata hata kama tutachelewa kujibiwa tusiache kumuomba Allaah, amesema mtume  s.a.w
"‏ مَا مِنْ أَحَدٍ يَدْعُو بِدُعَاءٍ إِلاَّ آتَاهُ اللَّهُ مَا سَأَلَ أَوْ كَفَّ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهُ مَا لَمْ يَدْعُ بِإِثْمٍ أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ ‏"

''Hakuna Yeyote anaeomba dua ispokuwa Allaah humpa alichoomba au humzuilia shari(jambo baya)lisimkute maadam hajaomba jambo baya au hajomba kukata udugu''

Yaan wewe umemuomba Allah akuwezeshe kupata ajira fulani uliyoona itakufaa badala yake ukaona unazidi kuchelewa kuipata kazi hiyo basi usiache kumuomba kwani kuna jambo baya mungu amekuepushia pengine kwenye kazi hiyohiyo ungefikwa na majuto ya maisha yote.

Katika hadithi inayosimuliwa na ibn Abbas r.a kwamba mtume s.a.w alikuwa akisema wakati wakati wa dhiki ,tatizo maneno yafuatayo:-


  "‏ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ الْعَظِيمُ الْحَلِيمُ، لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ، لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ رَبُّ السَّمَوَاتِ، وَرَبُّ الأَرْضِ، وَرَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ ‏"

Matamshi ya maneno haya ni kama ifuatavyo:-
  ‏‏"Laa ilaaha illa llaahul adhiymul haliym, Laa ilaaha illal-laahu Rabbul-l-'arsh il-'adhwiim, Laa ilaaha illa-llaahu Rabbu-s-samaawaati wa Rabbu-l-ardhwi, Wa Rabbu-l-'arsh-il-Karim."

Soma maneno haya kwa idadi kubwa na mara kwa mara ukiwa na dhiki, tatizo ama shida yoyote inayokusumbua , jambo hilo linalokusunbua ni kubwa kwako ama kwa binaadamu wenzako lakini ni jepesi mno kwa Allaah kukuondolea jambo hilo.

UKIWA NA SHIDA NA HUZUNI

Iwapo unasumbuliwa na huzuni,dhiki,shida, madeni,uvivu,kushindwa kufanikiwa malengo yako n.k fululiza kusoma utaratibu huu mara kwa mara kwa mara Inshaa Allaah hali itabadilika.


"‏ اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْهَمِّ وَالْحَزَنِ، وَالْعَجْزِ وَالْكَسَلِ، وَالْجُبْنِ وَالْبُخْلِ، وَضَلَعِ الدَّيْنِ، وَغَلَبَةِ الرِّجَالِ ‏"‏‏
Matamshi ya maneno haya ni kama ifuatavyo:-

Allaahumma inniy audhubika minalhammi walhazan, wal`ajzi walkasal,waljubni walbukhli, wadhwala`id dayn waghalabatir rijaal. 

Ndugu Msomaji pia tunaomba mchango wako katika kuwezeshe juhudi zetu hizi za kulingania waja wa Allah nawe utakuwa na sehemu ya kheri/ thawabu itakayopatikana  changia kupitia Tigo Pesa Namba 0715604488

Ndugu yangu kwa leo tuishie hapa mambo mengine mengi yanafuata, tumuombe mungu ajaalie juhudi hizi ziwe zimekubaliwa kwa ajili  ya kufuata radhi zake na atuepushe na shirki na kila balaa Inshaa Allaah.

.‏