KWA SILAHA HIZI SHETANI HANA AMANI

Assalaamu alaykum
Ndugu msomaji,

Baada ya kujua namna ya kusoma kisomo hiki ambacho ni maalumu kwa kupambana na mashetani,uchawi na husda. ni vyema kama utafahamu kuwa mgonjwa anasumbuliwa na shetani anaweza akapanda kwa mgonjwa ama ukaona dalili za kudhihiri kwake kama vile:-
1)kupiga miayo 2)kutikisika mwili 3)kusinzia 4)kutaka kutapika au kutapika (hii ni dalili ya kuathiriwa na uchawi) n.k hizi ni dalili utakazoziona wewe msomaji ambazo tunaziita ni dalili za wazi,



Lakini pia zipo dalili za siri ambazo huwezi kuzijua mpaka utakapo muuliza mgonjwa .
Endapo atakueleza mojawapo ya dalili zifuatazo:-
1)kutembea vitu mwilini,2)kuhisi maumivu ya kichwa 3) kuhisi joto au baridi kali 4)kuhisi kama amewekewa tofali kichwani (hali ya kuwa umemuwekea mkono tu) n.k


AYA ZA KUBATILISHA (KUUHARIBU) UCHAWI.


Utahitajika kumsomea mgonjwa aya za kubatilisha uchawi endapo
utamuona mgonjwa anapatwa na hali ya kutapika wakati wa kisomo, aya hizo ni kama ifuatavyo:-
utasoma suuratul A'araf aya ya 117-122

 وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَلۡقِ عَصَاكَ‌ۖ فَإِذَا هِىَ تَلۡقَفُ مَا يَأۡفِكُونَ (١١٧) فَوَقَعَ ٱلۡحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ (١١٨) فَغُلِبُواْ هُنَالِكَ وَٱنقَلَبُواْ صَـٰغِرِينَ (١١٩) وَأُلۡقِىَ ٱلسَّحَرَةُ سَـٰجِدِينَ (١٢٠) قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (١٢١) رَبِّ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ (١٢٢)    Utasoma hii mara 3 na sehemu hii   وَأُلۡقِىَ ٱلسَّحَرَةُ سَـٰجِدِينَ  utarudia mara 70

kisha utasoma suurat Yuunus aya ya 81-82

 فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئۡتُم بِهِ ٱلسِّحۡرُ‌ۖ إِنَّ ٱللَّهَ سَيُبۡطِلُهُ ۥۤ‌ۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُصۡلِحُ عَمَلَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ (٨١) وَيُحِقُّ ٱللَّهُ ٱلۡحَقَّ بِكَلِمَـٰتِهِۦ وَلَوۡ ڪَرِهَ ٱلۡمُجۡرِمُونَ (٨٢) utasoma mara 3 na sehamu hii  إِنَّ ٱللَّهَ سَيُبۡطِلُهُ ۥۤ‌ۖ   utarudia mara 33

 kisha suurat Twaha aya ya 69-70
وَأَلۡقِ مَا فِى يَمِينِكَ تَلۡقَفۡ مَا صَنَعُوٓاْ‌ۖ إِنَّمَا صَنَعُواْ كَيۡدُ سَـٰحِرٍ۬‌ۖ وَلَا يُفۡلِحُ ٱلسَّاحِرُ حَيۡثُ أَتَىٰ (٦٩) فَأُلۡقِىَ ٱلسَّحَرَةُ سُجَّدً۬ا قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ هَـٰرُونَ وَمُوسَىٰ (٧٠) utasoma mara 3 na sehemu hii وَلَا يُفۡلِحُ ٱلسَّاحِرُ حَيۡثُ أَتَىٰ  utarudia mara 33
 
KISHA UTASOMA AYAATUS SHIFAA

Baada ya kumsomea mgonjwa ayaatu ibtwaalis sihri inafaa kumsomea aya za kumuomba ALLAAH amponye mgonjwa kwani yeye ni muweza juu ya jambo hilo na aya zenyewe ni kama ifuatavyo:- 
 Suuratu tauba aya ya 14
قَـٰتِلُوهُمۡ يُعَذِّبۡهُمُ ٱللَّهُ بِأَيۡدِيڪُمۡ وَيُخۡزِهِمۡ وَيَنصُرۡكُمۡ عَلَيۡهِمۡ وَيَشۡفِ صُدُورَ قَوۡمٍ۬ مُّؤۡمِنِينَ
rudia mara 7

Suuratun Nahli aya ya 68-69
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨) ثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ فَٱسۡلُكِى سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلاً۬‌ۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٌ۬ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٲنُهُ ۥ فِيهِ شِفَآءٌ۬ لِّلنَّاسِ‌ۗ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَةً۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ rudia aya hizi mara 7

Suuratis Shu'araa aya ya 80  وَإِذَا مَرِضۡتُ فَهُوَ يَشۡفِينِ rudia mara 33

Suuratul Israa-il aya ya 82 
 وَنُنَزِّلُ مِنَ ٱلۡقُرۡءَانِ مَا هُوَ شِفَآءٌ۬ وَرَحۡمَةٌ۬ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ‌ۙ وَلَا يَزِيدُ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا خَسَارً۬ا 
 rudia mara 7


DAWA YA VITIMBI VYA SHETANI NA WACHAWI

 Kuna kipindi unaweza kufanyiwa vitimbi na shetani kama vile kumlaza mgonjwa ili asisikie kisomo, kupiga kelele na hata kumtisha msomaji mara nyingine hata kumtukana ukiona unafanyiwa hivyo na vitimbi vinginevyo vya wachawi soma aya zifuatazo bi idhni llah vitaondoka na shetani ataacha vituko vyake kumbuka kuwa hupaswi kuwa na jazba au kujipa mamlaka kwa mfano kusema "nitakukomesha leo" n.k

Suurat Aali Imraan aya ya 54     وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ  rudia mara 33

Suuratul Anfaal aya ya 30

وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ يُخْرِجُوكَ ۚ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ  rudia mara 33

Suurat Ibrahim aya ya 46

وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِندَ اللَّـهِ مَكْرُهُمْ وَإِن كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ  rudia mara 33

Suuratun Namli aya ya 50-51
وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٥٠ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ مَكْرِهِمْ أَنَّا دَمَّرْنَاهُمْ وَقَوْمَهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٥١
rudia mara 33
N.B idadi si sharti bali ni pendekezo kutokana na uzoefu Inshaa ALLAAH ukiwa na maswali,maoni au ushauri usikose kuwasiliana nami kwa simu namba +255715604488 

  Ndugu Msomaji tunaomba mchango wako ili utuwezeshe kutoa kitabu cha dua za tiba na kinga ambacho kimesheheni shuhuda na mawaidha mbalimbali ni kitabu kitakachowasaidia, kuwaelimisha watu wengi zaidi, Toa sadaka yako sasa na wewe uingie katika watakaopata thawabu za watakaoongoka kutoka katika ushirikina na maovu mbalimbali, gharama za uchapaji wa kitabu ni kubwa hivyo msaada wako ni muhimu tuchangie kwa njia zifuatazo:-
 TIGO PESA No. 0715604488 M-PESA No. 0758293138 
kwa wale wasomaji wetu wa nje ya nchi wawasiliane nami kwa simu na whatsapp namba +255715604488