Assalaamu alaykum.
Ndugu Msomaji leo nimeona nikueleze madhara ya kupona au kufanikiwa kulikopatikana kwa njia za kishirikina, Lakini kabla sijaigusa mada hiyo moja kwa moja napenda nikujulishe kwamba unaweza kusomewa/kutibiwa ukihitaji popote pale ulipo Duniani iwapo utakuwa tayari kugharamia nauli ya kuja huko na kurudi na gharama nyinginezo maana nimekuwa nikipigiwa simu na wasomaji wangu kutoka sehemu mbalimbali nchini,barani Afrika,Asia na Ulaya wakitaka kujua kama naweza kuwafuata huko, anayehitaji anaweza kunipigia kwa namba +255(0)715604488. Pia niwapongeze wale wote waliofuata taratibu mbalimbali nilizozielekeza na wamefanikiwa sifa njema na wa kushukuriwa kwa yote ni ALLAH pekee.
Ndugu Msomaji tunaomba mchango wako ili utuwezeshe kutoa kitabu cha dua za tiba na kinga ambacho kimesheheni shuhuda na mawaidha mbalimbali ni kitabu kitakachowasaidia, kuwaelimisha watu wengi zaidi, Toa sadaka yako sasa na wewe uingie katika watakaopata thawabu za watakaoongoka kutoka katika ushirikina na maovu mbalimbali, gharama za uchapaji wa kitabu ni kubwa hivyo msaada wako ni muhimu tuchangie kwa njia zifuatazo:-
TIGO PESA No. 0715604488 M-PESA No. 0758293138
kwa wale wasomaji wetu wa nje ya nchi wawasiliane nami kwa simu na whatsapp namba +255715604488
Ndugu Msomaji tunaomba mchango wako ili utuwezeshe kutoa kitabu cha dua za tiba na kinga ambacho kimesheheni shuhuda na mawaidha mbalimbali ni kitabu kitakachowasaidia, kuwaelimisha watu wengi zaidi, Toa sadaka yako sasa na wewe uingie katika watakaopata thawabu za watakaoongoka kutoka katika ushirikina na maovu mbalimbali, gharama za uchapaji wa kitabu ni kubwa hivyo msaada wako ni muhimu tuchangie kwa njia zifuatazo:-
TIGO PESA No. 0715604488 M-PESA No. 0758293138
kwa wale wasomaji wetu wa nje ya nchi wawasiliane nami kwa simu na whatsapp namba +255715604488
MADHARA YA KUPONA AU KUFANIKIWA KWA NJIA ZA KISHIRIKINA
Mpendwa msomaji yapo madhara mengi yanayoweza kumpata mtu aliepona maradhi kama vile ya Kishetani au Uchawi baada ya kutibiwa kwa njia za kishirikina au aliyepata utajiri/ kazi kwa njia za kishirikina, haya ni madhara machache miongoni mwa madhara mengi anayoweza kupata mtu huyo.
KUHARAMISHIWA PEPO/KUTOINGIA PEPONI.
Hii ni kwa maneno ya mwenyezimungu mtukufu ambaye ndiye aliyetuumba sote na kila kitu
إِنَّهُ ۥ مَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ ٱلۡجَنَّةَ وَمَأۡوَٮٰهُ ٱلنَّارُۖ
"wani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni"
Sasa ndugu msomaji kuna jambo zuri kama mtu kupata pepo na ubaya ulioje kwa atakayeikosa pepo maana atakuwa na makazi ya kudumu motoni
KUYATUMIKIA MASHETANI MAISHA YAKO YOTE.
Madhara mengine yanayomkabili mtu huyu ni ya kidunia ambapo hulazimika kama alipata mtoto baada ya kufanyiwa tiba za kishirikina kuna masharti huwa anapewa labda jina la mtoto atachaguliwa na shetani husika na kutakiwa kufungwa mahirizi makambakamba mbalimbali mwilini na pia hutakiwa mtoto husika akabidhiwe kwa shetani(mwalimu). vyote hivi ni haramu mwanaadamu hatakiwi kukingwa na shetani wala hirizi bali kuna taratibu maalum zilizofundishwa na Mtume S.a.W namna ya kujikinga dhidi ya shari mbalimbali.
MADHARA YA ALIYEPATA UTAJIRI/KAZI KWA NJIA ZA KISHIRIKINA.
Na hapa kuna mtihani mkubwa utakuta mtu hana maisha mazuri anawasikia watu wanamsifu mganga (mtaalamu) fulani kuwa ana dawa za utajiri na yeye bila kujishauri anakimbilia tu huko ( na sasa wamejaa sana wenye kuwapa watu njia za kupata pesa za majini).
Na kwa tamaa ya maisha mazuri aliyonayo hujikuta lolote atakaloambiwa na mganga yeye ni tawire tu hana la kukataa hata moja na hapo mtu huyu yupo tayari kutekeleza chochote hata kama ni kutembea (kuzini) na mama yake mzazi, mwanawe wa kumzaa n.k yupo tayari hata kama ni kwa kubaka na ikiwa atatakiwa kuua ataua tu, pamoja na hayo ambayo yote yanamchukiza Mwenyezimungu bado anakumbana na masharti magumu ya kutokula wala kuvaa vizuri pamoja na utajiri alionao!
Mwingine anakula vibandani tu hata iwe sikukuu, nguo anazovaa ni kuukuu na yale aliyoyafanya wakati anautafuta huo utajiri hutakiwa kuyarudia kila baada ya muda fulani (kuzini,kuua,kufanya zezeta watu wa karibu) baadhi yetu ni mashahidi wa haya ninayoyasema mitaani mwetu.
Mwingine hupewa masharti ya kuchinja kila baada ya muda fulani eti hutoa sadaka na asipofanya hivyo mambo humuharibikia wakati kuchinja ni katika ibada za kuabudiwa ALLAAH S.W.T pekee.
Mpendwa msomaji wangu haya ni machache tu miongoni mwa mengi yanayowakabili waliofanikiwa kiafya ama kimali kwa kufuata njia za kishirikina nakuusia ndugu yangu hapa Duniani ni njiani tunaelekea kwenye makazi ya kudumu, ambayo kuna hasara kubwa kwa atakayekwenda na dhambi za ushirikina na kuna faida kubwa kwa atakaejiepusha na ushirikina.
Mpaka kufika hapa napumzika EWE MWENYEZIMUNGU SHUHUDIA KUWA NIMEWAFIKISHIA WAJA WAKO.
"Amani iwe kwa atakeufuata uwongofu"