MAONI/USHAURI NA MASWALI YA WASOMAJI

Wapendwa Wasomaji wangu
Assalaam alaykum.
Kwanza kabisa napenda nichukue fursa hii kumshukuru Allah kwa kutujaalia kuwa miongoni mwa walioidiriki Ramadhwaan ya mwaka huu 1434/2013 kwani wapo wengi waliopenda kufunga mwaka huu lakini imeshindikana ima kwa kufikwa na umauti ama kwa kushikwa na maradhi.
Namuomba Mungu atujaalie funga zetu ziwe ni zenye kukubaliwa hatimaye tufikie lengo kuu la funga Inshaa Allah.kuanzia sasa tutakuwa tunawaletea maoni/ushauri na maswali mbalimbali na majibu yake kutoka kwa wasomaji wa blog hii ya Tiba Sahihi.

Kuna msomaji wangu kutoka IRINGA MUFINDI anasema;-
''....nipo iringa mufindi ,je kama nataka nifanikiwe kwa njia ya shetani nitakupataje wakati nipo mbali na wewe?''
JIBU kutoka Tiba Sahihi: Ndugu yangu kwanza kabisa nakukumbusha kuwa lengo kuu la kuanzisha blog hii ni kupinga na kupambana na imani za kishirikina na kishetani kwa namna yoyote ile hivyo hakuna njia ya kishetani utakayoelekezwa humu uitumie ili ufanikiwe kwa kupata mali, afya ,kazi,mume/mke, upendo na maelewano ispokuwa ni kwa kufuata taratibu za halali ambazo pia zitakuweka karibu na Mwenyezimungu.

Msomaji mwingine kutoka TANGA,LUSHOTO,SONI anasema;-
''A.alaykum,Allah akulipe wema Duniani na Akhera kwa kuweka BLOG ya kuwasaidia wenye matatizo ya kisaikolojia kama vile UCHAWI, MASHETANI n.k mimi ni ndugu yko ktk imani kutoka TANGA LUSHOTO SONI Naitwa Hassan Abdallah. Nami ni muathirika wa matatizo hayo(sihir na mashetani) kuanzia 2010,Alhamdulillahsasa hivi napata nafuu taratibu kwa kusoma kutoka moyoni aya za kubatilisha uchawi.Ahsante sana na SWAUMU NJEMA''
JIBU kutoka Tiba Sahihi: W' salaam ndugu yangu katika imani na s shukran ni za mwenyezimungu kw akujaalia hali hiyo uliyo  kuwa nayo baada ya kufuata utaratibu ulioelekezwa humu kwenye hii BLOG  na ni juu yako kuhakikisha kuwa unadumu na utaratibu huu mpaka hapo Allah atakapokuponya kabisa maradhi yako Inshaa Allah.

Maoni na maswali yapo mengi lakini kwa leo nimefanikiwa kuyajibu machache kutokana na ufinyu wa fursa lakini nitaendelea kuyajibu katika post ijayo Inshaa Allah, na wewe ukiwa na maoni , ushauri au maswali unaweza kunitumia kwenye namba yangu hapo juu au kunitumia kwenye email hii palike83@gmail.com