ANGALIZO MALIPO YA KUFUNGA SIKU 29/30 YANAWEZA KUHARIBIKA SIKU MOJA TU.

Ndugu msomaji, 

Leo kidogo nimeona nibadilike katika mada zangu kwa ajili ya kuwakumbusha Waislam wenzangu juu ya sherehe za sikuu ya EID ili waweze kulinda malipo ya swaumu zao  kwani wengi wetu wameghafilika. 

Assalaam alaykum
Ndugu Muislam,
Umejitahidi na kwa msaada wa ALLAH huenda ukamaliza funga ya siku 29/30, iwapo utawafikishwa kuidiriki EID ELFITR ni bora ukaepuka kumuasi ALLAH kwenye SHEREHE hizo, epuka kuvaa nguo zinazoonyesha maungo yako kumbuka kuwa uchi wa mwanamke ni mwili wake wote ispokuwa uso na viganja vya mikono HIVYO HUPASWI KUACHA WAZI SEHEMU HIZO,Epuka ULEVI,KUMBI ZA MUZIKI(IKIWEMO KUIMBA,KUCHEZA,NA KUPIGA), ZINAA n.k kwani kufanya hayo ni hatari sana na MTUME SWALLA LLAAHU `ALAYHI WASALLAM AMESEMA, ANAEMUASI ALLAAH SIKU YA SIKUKUU (EID) NI KAMA AMEMUASI SIKU YA HUKUMU (KIAMA) EWE ALLAAH SHUHUDIA KUWA NIMEWAKUMBUSHA WAJA WAKO. WASSALAAMU `ALAA MANIT TABA`ALHUDAA.