UVUMILIVU NI MUHIMU KATIKA KUTAFUTA PONYO
Assalaam alaykumNdugu Msomaji
Kabla ya kuanza somo la leo nichukue nafasi hii kuwaombea wagonjwa na wenye shida na matatizo mbalimbali waliopo sehemu mbalimbali duniani hususan Dada yangu katika Iman ambaye yupo nchini Sweden kwani baada ya kusoma blog hii na kupata namba yangu walinitafuta na kunielezea matatizo yanayo wakabili namuomba Allah S.W.T amfanyie wepesi kuondokana na matatizo yanayomkabili na awape subra wanaomuuguza akiwemo mumewe Inshaa Allaah , na wengineo kutoka sehemu mbalimbali.
Leo nimeona ni bora nikazungumzia suala zima la uvumilivu kwa kila mgonjwa na mwenye hitajio aratibu wa usiokuwa wa kishirikina katika kutafuta suluhisho la matatizo yanayomkabili,
Ni vizuri watu wakaelewa kwamba katika kumuomba mungu akuondolee dhiki zinazo kukabili inawezekana kukachukua muda mrefu mpaka kupata suluhisho la matatizo yako, Kuna ambao humuomba mungu kwa kipindi kirefu lakini majibu yanachelewa kupatikana hapo utakuta mtu asie na msimamo anabadilika na kuanza kutafuta njia mbadala za kufikia lengo lake na hapo hujikuta akiingia katika kumuasi Allaah, na kwa kufanya hivyo wapo wanaofanikiwa ili Allaah apate kuwaadhibu vizuri hapa duniani ama hapo akhera.
Wengine hutarajia kupata ponyo la haraka baada ya kugeukia upande huu wa tiba sahihi ni vizuri lakini la muhimu ni kuwa nayakini kuwa unaemuomba sio kiziwi anakusikia na anakuona na anajua hali yako kabla hujamuomba.
Wakati mwingine Allaah hupenda kumuona mja wake akimuomba kila mara kwa kila hitajio kwani yeye hufurahi anapoombwa na huchukia mno asipoombwa, je vipi ukiacha kumuomba yeye na kumuomba kiumbe?
Mtume Mussa A.S Alipomuomba mungu juu ya kuangamizwa kwa fir`aun na watu wake wana wazuoni wanasema ilichukua miaka 40 mpaka kujibiwa kwa ombi hilo hivyo kuchelewa kujibiwa ama kuonywa maradhi yako sio kwamba mungu amekukasirikia bali mungu anaendelea kukupima imani yako je utatetereka? ama utaendelea kuwa na msimamo?
Nikiwa katika kazi hii ya tiba nimewahi kuwafanyia visomo watu wenye shida na matatizo mbalimbali ambapo wengi wao walikuwa wameshapitia kwenye ushirikina bila mafanikio na miongoni mwao kuna dada mmoja anatokea kimara yeye kwa kinywa chake amepata kunihadithia mbele ya wagonjwa wenziwe kwamba alishachinjiwa ng`ombe na kuchimbiwa mpaka kaburi lakini hakuna mafanikio aliyoyapata lakini kwangu alikuwa anakuja kila siku kwa kipindi cha zaidi ya miezi 6 huku mabadiliko yakipatikana kidogo kidogo na hatimae kupona kabisa maradhi yake bila ya kuchinjiwa ng`ombe wala kuchanjwa chale hayo yalitokea kwa REHMA ZA ALLAAH wala sio uhodari wa Hemedi Palike.
La mwisho na la muhimu ninalowausia wasomaji wangu ni kuwa na subra mwenyezimungu atakuwa pamoja nanyi INSHAA ALLAH, WASSALAAMU `ALAA MANIT TABA`ALHUDAA.