VISOMO SASA KUPATIKANA KWA NJIA YA SIMU

Wasomaji wangu Wapendwa 
Assalaam alaykum

Kutokana na maombi ya wasomaji wengi nimeona ni vyema nikaanzisha utaratibu maalum wa kuwasomea dua kwa njia ya simu wagojwa na wahitaji mbalimbali  walio mbali haswa wale wa nje ya nchi ambao gharama za kufika
huko walipo ni kubwa na wanahitaji kupatiwa huduma hii.

Hivyo wale wanaohitaji wanaweza kuwasiliana nami tukapanga utaratibu wa namna ya kutumia mfumo huu huku pia tukizingatia time (saa) za hapa nyumbani na kule anapoishi muhitaji.

Pia kuanzia sasa utaweza kutumiwa madawa  kutokana na mahitaji yako iwapo utalipia gharama za kuandaliwa hizo dawa dawa pamoja na gharama za usafiri mpaka hapo ulipo.

Naamini fursa hii itachangamkiwa na wale wote waliokuwa wakisononeka kwa kukosekana kwake. Nawatakia Shughuli njem za ujenzi wa mataifa yenu na kila la kheri katika Maisha yenu.