HAYA NI BAADHI YA  NILIYOYASHUHUDIA KWENYE KAZI HII No-1


Assalaam alaykum
Msomaji Wangu Mpendwa

Kwanza kabisa Namshukuru Allaah S.W.T  alietuumba na kutufanyia mengi tuyapendayo kwa rahma zake nashuhudia kuwa yeye ndiye aliniumba mimi na wengineo na vyote vilivyomo mbinguni na ardhini na yeye pekee ndie apasaye kuabudiwa,kuombwa na kukimbiliwa kwa shida
na dhiki mbalimbali. Nashuhudia pia Muhammad S.a.W ni mja wake na ni mtume wake wa mwisho kwa walimwengu wote, Rahma na amani ziwe juu yake yeye, familia yake, maswahaba zake na wote watakaofuata mwongozo wake mpaka siku ya kiama.

Nawashukuru wasomaji wangu kutoka nchi mbalimbali ambao wamekuwa wafuatiliaji wakubwa wa masomo mbalimbali huku wengi wao wakinipigia simu kunipongeza ama kutaka kujua zaidi na wengine wakiwa ni wahitaji wa dua kwa shida zao mbalimbali.

Zaidi wasomaji wangu wa Canada, Sweden, Holand,United Kingdom,Oman, Kenya na bila kusahau nyumbani Tanzania, niwaambie tu kuwa nawakaribisha na msichoke kunipigia pindi muwapo na shida ama mkipenda kuwasiliana nami,

Leo nimependa kuwaeleza ndugu zangu mambo mbalimbali niliyokutana nayo katika kuonyesha maajabu ya Qur`aan na Adhkaar mbalimbali katika kuondosha shida na matatizo mbalimbali kwa idhini ya Allaah.

  1. MTOTO ALIEKUWA AKIBADILIKA RANGI MARA TU ASHIKWAPO NA MAMA YAKE                                                                                                                                                                                                                             Hii ilikuwa ni Ramadhwan ya mwaka 2011 aliletwa mtoto mchanga mwenye umri wa kati ya miezi 3 au 4 akiwa amebebwa na bibi yake ambaye wakati huo alikuwa ndio mlezi wake, wakanieleza kuwa huyo mtoto hamtaki mama yake na kama akimshika analia sana na anabadilika rangi na kuwa wa manjano hivyo tangu walipoona hivyo mtoto huyo hakai na mama yake, Nilichokifanya nilimsomea dua mama yake na kusomea maji ya kunywa na kumwambia mama yake amchukue mwanawe mwanzo mama mtu aliogopa lakini nikamsisitiza amtaje Allaah na kuna adhkaar nilimsomesha na alipomchukua, kwaidhini ya Allaah mtoto hakulia wala hakubadilika rangi tena, hizi zilikuwa ni fadhila za Allaah kwa waja wake.                                                                                                     
  2. AKOSA AMANI NA USINGIZI KILA IFIKAPO USIKU                                                                                                                                          Huyu ni kijana wa kiume ambaye ni fundi alikuja ofisini kwangu kwa ajili ya kufanya marekebisho madogona ilipofika wakati waa jioni ghafla akaanza kubadilika na nilipo mdadisi kwanini yupo vile akaanza kunisimulia hali ya kukosa amani na usingizi kila ufikapo wakati wa usiku na hali hiyo imekuwa ikimsumbua kwa kipindi kirefu na bado hajapata suluhisho la tatizo hilo. nikamtaka asiwe na wasiwasi na atawakkali kwa Allaah kwani tatizo lake siku hiiyo limefikia mwisho kwa idhini ya Allaah hii ilikuwa ni Ramadhwaan ya mwaka 2012 na wakati huo ilikuwa imeshafikia mwishoni hivyo tulikuwa tumefunga ofisi kwa muda wa siku 10 kupisha sikuu na mfungo wa 6 lakini huwa nina utaratibu wa kuwaaandalia wagonjwa mafuta maalum ya kutumia kwa siku hizo za mapumziko hivyo sehemu ya mafuta hayo yalikuwa yamebaki, nikamtaka yule kijana ayatumie kwa kupaka usiku ule na kila siku apake asubuhi na usiku, Alhamdulillaah yule kijana akafuata utaratibu huu na baada ya wiki nikaonana nae akanieleza kuwa tatizo lilokuwa likimsumbua kwa muda mrefu halipo tena hizi ni katika fadhila za ALLAAH yeye ni muweza juu ya kila kitu.


 NAWASHAURI WAPENZI WASOMAJI WANGU TUWE TUNAWEKEANA NIA KWENYE DUA

Hili ni jambo dogo lakini lina faida na lina umuhimu mkubwa sana nikiwa ofisin nimekuwa na utaratibu wa dua maalum siku moja katika wiki na nimekuwa nikiwashauri watu ninaokuwa nao kwenye dua wawekeane nia, yani wakati ukijiwekea nia juu ya tatizo lako unawakusudia na wengine Allaah awafanyie wepesi kufanikiwa wanayoyatamani au kuepushwa wanayoyahofia na mwisho wa siku pamoja na kupata thawabu lakini pia unaweza kuitikiwa na kufanikiwa kwa nia yako njema juu ya mwenzako.

Miongoni mwa wasomaji wanaowasiliana nami kutoka zaidi ya nchi 7 wapo wenye shida mbalimbali wakimuomba Allaah awafanyie wepesi na kuwaondolea vikwazo katika kuyafikia wanayoyataka, wengine kazi, Afya , Makazi, Mahusiano (mke & mume) na wengine maradhi.

Hivyo kuanzia jumatano hii ya tarehe 16/10/2013 nawashauri wasomaji wangu tupate kusoma aya hii ya Qur`aan 
وَمَا ذَٲلِكَ عَلَى ٱللَّهِ بِعَزِيزٍ
 WAMAA DHAALIKA `ALA LLAAHI BI`AZIIZ  kwa idadi kubwa na kila mmoja popote alipo duniani akusudie kumuomba Allaah kuondolea jambo analolihofia ( kama ugonjwa,chuki,mashaka n.k) ama ampatie analolitaka ( kama ajira,kupanda vyeo,kuwashinda maadui n.k) na amuwekee nia kama hiyo kila muhitaji popote alipo dunia.

Pia napenda kuwataarifu wasomaji wangu kuwa sina utaratibu wa ku update post mara kwa mara kwa kuwa haya niyaandikayo si hadithi za kutunga bali ni mambo halisi yanayowakuta watu wote hivyo nakusudia kuwafikishia wasomaji wote, ndio maana naziacha muda mrefu ili watu wazifanyie marejeo katika matukio yao ya kila siku, kusudio kuu likiwa ni kutafuta radhi za Allaah ili anirehem kwa rahma zake Inshaa Allaah.