KISA CHA MASIKINI CHENYE MAZINGATIO -2
 



Msomaji Wangu Mpendwa
Assalaam alaykum
 
Kwanza kabisa hatuna budi kumshukuru Mungu Wa Pekee aliyeumba kila kitu asiyefanana na  yeyote wala chochote kwa kutuwezesha kuwa pamoja tena katika Mtandao Wetu Bora kabisa Wa Tibasahihi tukielimishana mambo mbalimbali yenye kutufaa katika dunia na akhera yetu Pia tumtakie ziada ya Rehma na Amani Mtume Wetu Muhammad S.A.W na Aali zake na Sahaba zake na wote watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya malipo.
 
Leo tunaendelea na Sehemu Ya 2 Na Ya Mwisho Ya Kisa Cha Masikini Chenye Mazingatio Makubwa.

Baada ya Kupita Muda Mrefu Yule Malaika Akarudi Kwa Wale Masikini watatu ambao pia walikuwa na maradhi mbalimbali, Wa kwanza kufuatwa alikuwa yule yule alikuwa wa kwanza kusaidiwa huyu alikuwa na ugonjwa wa ngozi (Malaika) alipofika kwake (Akiwa katika muonekano ule ule wakati alipokuja kumsaidia) akamwambia mimi ni msafiri niliyeharibikiwa katika safari yangu na hakuna wa kunifikisha katika safari yangu ispokuwa kwa msaada wa Mwenyezimungu Kisha Msaada wako, nakuomba kwa (haki) ya yule aliyekupa ngozi na rangi nzuri na akakupa na ngamia, nakuomba mnyama mmoja atakayenifikisha katika safari yangu. Akajibu hakika nina majukumu mengi sana, Yule Malaika Akamuuliza hukuwa na ugonjwa wa ngozi wa wanakutenga? Masikini Kisha Allah akakuponya na akakupa mali?  akajibu hakika nimerithi mali hizi kutoka kwa mababu zangu. Basi Yule malaika akamwambia kama ikiwa ni muongo basi Mwenyezimungu akurudishe katika hali uliyokuwa nayo mwanzo.

Wa Pili kufuatwa alikuwa yule yule aliyekuwa wa Pili kusaidiwa huyu alikuwa na ugonjwa wa kutoota nywele (Malaika) alipofika kwake (Akiwa katika muonekano ule ule wakati alipokuja kumsaidia) akamwambia mimi ni msafiri niliyeharibikiwa katika safari yangu na hakuna wa kunifikisha katika safari yangu ispokuwa kwa msaada wa Mwenyezimungu Kisha Msaada wako, nakuomba kwa (haki) ya yule aliyekupa nywele nzuri na akakupa na Ng'ombe, nakuomba mnyama mmoja atakayenifikisha katika safari yangu. Akajibu hakika nina majukumu mengi sana, Yule Malaika Akamuuliza hukuwa na ugonjwa wa ngozi wa wanakutenga? Masikini Kisha Allah akakuponya na akakupa mali?  akajibu hakika nimerithi mali hizi kutoka kwa mababu zangu. Basi Yule malaika akamwambia kama ikiwa ni muongo basi Mwenyezimungu akurudishe katika hali uliyokuwa nayo mwanzo.

Wa tatu kufuatwa alikuwa yule yule aliyekuwa wa tatu kusaidiwa huyu aliyekuwa na ugonjwa wa ngozi (Malaika) alipofika kwake (Akiwa katika muonekano ule ule wakati alipokuja kumsaidia) akamwambia mimi ni msafiri niliyeharibikiwa katika safari yangu na hakuna wa kunifikisha katika safari yangu ispokuwa kwa msaada wa Mwenyezimungu Kisha Msaada wako, nakuomba kwa (haki) ya yule aliyekurudishia macho yako na akakupa na ngamia, nakuomba mnyama mmoja atakayenifikisha katika safari yangu. Akamwa ni kweli nilikuwa Kipofu Allah akanirudishia Macho yangu na nilikuwa masikini Allah akanipa mali hivyo basi chukua utakacho na uache utakacho sitakuzuia kwa chochote utakachochukua. basi yule malaika akamwambia baki na mali zako hakika nyinyi (watatu) mlipewa mtihani na mwenyezimungu na amekuridhia wewe na amewachukia wenzako.
 
 
MAZINGATIO YALIYOMO KWENYE SIMULIZI HII
 
 Yafuatayo ni baadhi ya mazingatio yanayopatikana katika simulizi hii.
  1. Mwenyezimungu ana uwezo wa kubadilisha hali za viumbe wake hata hali zao zikiwa ngumu na mbaya kiasi gani
  2. Kubadilishwa hali kutoka katika maradhi na kuwa katika uzima na kutoka katika umasikini kuja katika utajiri pia kunaweza  kuwa ni mtihani anaopewa mja ili aangaliwe na Muumba wake kama atashukuru ama atakufuru, kushukuru ni kutoa katika kusaidia wasiojiweza,ujenzi wa misikiti,hospitali kuchimba visima n.k na kinyume chake ni kujizuia kutoa katika hivyo vilivyotajwa n.k
  3. Kutambua kuwa aliyekupa mtihani huo ni Allaah na yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kukuondolea kama alivyotambua hilo kipofu na hatimaye hata mwisho yeye kipofu ndiye aliyefaulu mtihan huu ukilinganisha na wenzake wawili waliofeli.           
Mpendwa Msomaji wangu ukiwa na swali,maoni ama ushauri  nifuatilie kupitia twitter kwa kuponyeza hapa https://twitter.com/HemediPalike