Huna Haja Ya Kufanya Ushirikina Ili Kufanikiwa Katika Biashara/Kazi
 QUR'AAN INAKUTOSHA SANA-01

Msomaji Wangu Mpendwa,
Assalaamu Alaykum,

Ndugu Msomaji tunaomba mchango wako ili utuwezeshe kutoa kitabu cha dua za tiba na kinga ambacho kimesheheni shuhuda na mawaidha mbalimbali ni kitabu kitakachowasaidia, kuwaelimisha watu wengi zaidi, Toa sadaka yako sasa na wewe uingie katika watakaopata thawabu za watakaoongoka kutoka katika ushirikina na maovu mbalimbali, gharama za uchapaji wa kitabu ni kubwa hivyo msaada wako ni muhimu tuchangie kwa njia zifuatazo:-
 TIGO PESA No. 0715604488 M-PESA No. 0758293138 
kwa wale wasomaji wetu wa nje ya nchi wawasiliane nami kwa simu na whatsapp namba +255715604488
Katika Maisha Binadamu Huwa tunahangaika katika kutafuta riziki kwa namna mbalimbali ili kutuwezesha kujikimu kwa mahitaji yetu ya kila siku,
Miongoni mwetu  wapo wanaofanya biashara lakini pia wapo wafanya kazi na katika hali zote hizi yaani kwa  wafanya biashara na wafanya kazi wamakuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali kutokana na hali ya walimwengu walivyo hivi sasa watu hufanyiana ubaya (kama kufanyiana uchawi ili
fulani asiuze niuze mimi)  

Na mtu anapoona mambo yake hayaendi sawa ima kwa kushawishiwa ama mwenyewe maisha yake yameshakuw ya namna hiyo ya kila kitu kwenda kwa waganga, basi ataelekea huko na pengine ataambiwa kafukie kitu hiki kwenye sehemu yako ya biashara au chukua hirizi hii ukae nayo kwenye biashara zako au kama mtu huyo ni muajiriwa basi atatakiwa kuwa nayo katika sehemu yake ya kazi. 


Pichani Bidhaa Zikiwa Sokoni Tayari Kwa Kuuzwa


Tunasema kwamba vitendo hivi vyote ni katika vitendo vya kishirikina na kwa kuviendekeza vitendo hivi ili upate mafanikio utakuwa tayari wakati mwingine hata kufanya vitendo vibaya zaidi kama kumfanya ndugu au mtoto zezeta, kutembea na wazazi, kuuwa au kumkata mkono albino ili mradi upate mafanikio,utajiri au madaraka nawasihi ndugu zangu kuwa vitendo vyote hivyo ni haramu na vinamchukiza sana Mwenyezi Mungu aliyekuumba wewe,mimi na hao unaowadhulumu Na kufanya hivyo ni kudhulumu haki yao ya kuishi wakiwa wamekamilika  viongo vyao vya mwili pia vinarudisha nyuma maendeleo ya jamii. 


Badala yake nakushauri kushika Qur'an ndio iwe mkombozi wako katika biashara, kazi zako na maisha yako ya kila kitu.
Na kuanzia sasa nitakuwa nakuletea mfululizo wa sura au aya za Qur'an unazoweza kutumia kwa ustawi wa shughuli zako kama ifuatavyo:- 

Ili kusoma Qur'an zingatia kuwa na udhu

Soma sura hii Kila Siku Asubuhi sehemu yako ya kazi.

بِسۡمِ ٱللهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
الٓمٓر‌ۚ تِلۡكَ ءَايَـٰتُ ٱلۡكِتَـٰبِ‌ۗ وَٱلَّذِىٓ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ ٱلۡحَقُّ وَلَـٰكِنَّ أَڪۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ (١)ٱللَّهُ ٱلَّذِى رَفَعَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ بِغَيۡرِ عَمَدٍ۬ تَرَوۡنَہَا‌ۖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ‌ۖ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ‌ۖ كُلٌّ۬ يَجۡرِى لِأَجَلٍ۬ مُّسَمًّ۬ى‌ۚ يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَ يُفَصِّلُ ٱلۡأَيَـٰتِ لَعَلَّكُم بِلِقَآءِ رَبِّكُمۡ تُوقِنُونَ (٢) وَهُوَ ٱلَّذِى مَدَّ ٱلۡأَرۡضَ وَجَعَلَ فِيہَا رَوَٲسِىَ وَأَنۡہَـٰرً۬ا‌ۖ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ جَعَلَ فِيہَا زَوۡجَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِ‌ۖ يُغۡشِى ٱلَّيۡلَ ٱلنَّہَارَ‌ۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ (٣)


Soma Sura Hii Mara 3 Kila Baaada ya Swala, Pia Unaweza kufanya hivyo katika sehemu yako ya kazi au biashara.

بِسۡمِ ٱللهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
أَلَمۡ نَشۡرَحۡ لَكَ صَدۡرَكَ (١) وَوَضَعۡنَا عَنكَ وِزۡرَكَ (٢) ٱلَّذِىٓ أَنقَضَ ظَهۡرَكَ (٣) وَرَفَعۡنَا لَكَ ذِكۡرَكَ (٤) فَإِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا (٥) إِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرً۬ا (٦) فَإِذَا فَرَغۡتَ فَٱنصَبۡ (٧) وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرۡغَب (٨)

Taratibu hizi ni ndefu na nitakuwa nawaletea vile nitakavyojaaliwa na Mwenyezi Mungu.
Ndugu Msomaji endelea na utaratibu huu katika maisha yako ya kila siku.

Kwa yeyote ambaye angependa  kufanyiwa kisomo cha aina hii na vinginevyo kwa haja mbalimbali wanaweza kuwasiliana nami kwa simu namba au Whatsapp +255715604488, Mafanikio bila Ushirikina Inawezekana.