KINGA YA KISHARIA DHIDI YA SHETANI

,UCHAWI,HUSDA NA KILA SHARI-1



 Msomaji Mpendwa Assalaamu alaykum,
Awali ya yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu alitujaalia kuwa hai katika muda huu na kutuneemesha kwa neema mbalimbali.

Pia tunaomba mchango wako ili utuwezeshe kutoa kitabu cha dua za tiba na kinga ambacho kimesheheni shuhuda na mawaidha mbalimbali ni kitabu kitakachowasaidia, kuwaelimisha watu wengi zaidi, Toa sadaka yako sasa na wewe uingie katika watakaopata thawabu za watakaoongoka kutoka katika ushirikina na maovu mbalimbali, gharama za uchapaji wa kitabu ni kubwa hivyo msaada wako ni muhimu tuchangie kwa njia zifuatazo:-
 TIGO PESA No. 0715604488 M-PESA No. 0758293138 
kwa wale wasomaji wetu wa nje ya nchi wawasiliane nami kwa simu na whatsapp namba +255715604488

Sasa turudi kwenye madayetu ya leo, Ndugu Msomaji tambua kuwa Uislam ni dini iliyokamilika katika kila idara inayohusu maisha ya viumbe na miongoni mwa mambo ambayo pia yanapatikana ndani ya uislam ni kinga ya kisheria dhidi ya kila shari kama vile shetani,uchawi,husda,kijicho n.k

Kinga hii ndiyo mujarrab na hupaswi kujikinga kwa hirizi wala chale kama wafanyavyo/wafanyiwavyo wengi miongoni mwa jamii ya wanaadamu na la kusikitisha zaidi katika kundi la wanaoamini na kufanya ushirikina huu ni waislam!
Ndugu zangu shirki ni jambo baya sana na ni miongoni mwa dhambi kubwa ambayo ALLAH amemuambia mtume wake kuwa

  وَلَقَدۡ أُوحِىَ إِلَيۡكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكَ لَٮِٕنۡ أَشۡرَكۡتَ لَيَحۡبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَـٰسِرِينَ  
 Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a'mali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri

Huyo ni mtume wa allaah vipi mimi na wewe?

Kwa kuzingatia hilo nimeona ni kheri leo nikawaletea taratibu sahihi za kujikinga ambazo unatakiwa udumu nazo kila siku asubuhi na jioni.

Ni matarajio yangu kwamba tutaendelea kuwa pamoja ili tuweze kufaidika na elimu hii ya bure kabisa kwa ajili ya kutafuta radhi ya ALLAH

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ


Laa Ilaaha Illa llaahu wahdahuu laa shariika lahu lahulmulku walahul hamdu wahuwa alaa kulli shai-in qadiir
mara 100 asubuhi na jioni

ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَىُّ ٱلۡقَيُّومُ‌ۚ لَا تَأۡخُذُهُ ۥ سِنَةٌ۬ وَلَا نَوۡمٌ۬‌ۚ لَّهُ ۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَا فِى ٱلۡأَرۡضِ‌ۗ مَن ذَا ٱلَّذِى يَشۡفَعُ عِندَهُ ۥۤ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦ‌ۚ يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡ‌ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَىۡءٍ۬ مِّنۡعِلۡمِهِۦۤ إِلَّا بِمَا شَآءَ‌ۚ وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ‌ۖ وَلَا يَـُٔودُهُ ۥ حِفۡظُهُمَا‌ۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِىُّ ٱلۡعَظِيمُ

Allaahu laa ilaaha illaa huwalhayyul qayyuum laa ta-akhudhuhuu sinatun walaa nauum lahuu maa fis samaawaati wamaafil-ardhwi man-dhalladhiy yashfa'u 'in-dahuu illaa bi-idhnihii ya'alamu maa baina aidiihim wamaa khalfahum walaa yhiitwuuna bishai-in min 'ilmihii illaa bimaa shaa-a wasi'a kursiyyuhus samaawaati wal-ardhwa walaa ya-uuduhuu hifdhuhumaa wahuwal'aliyyul'adhwiim. mara 1 kila baada ya swala ya fardhi

بِسۡمِ ٱللهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ (٢) لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ (٣) وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ ڪُفُوًا أَحَدٌ (٤)
 1)
Qul huwa llaahu ahadu. 2) allaahus swamadu. 3) lamyalid walam yuulad. 4) walam yakunlahuu kufuwan  ahad

mara 3 asubuhi na wakati wa kulala* 

بِسۡمِ ٱللهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ (١) مِن شَرِّ مَا خَلَقَ (٢) وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ (٣) وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَـٰتِ فِى ٱلۡعُقَدِ (٤) وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ (٥)
Qul a'uudhu birabbil falaq. minsharri maa khalaq. waminsharri ghaasiqin idhaa waqaba. waminsharrin n affaathaati fil'uqad. waminsharri haasidin idhaa hasada. mara 3 asubuhi na  wakati wa kulala*


بِسۡمِ ٱللهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١ مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢ إِلَـٰهِ النَّاسِ ﴿٣ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ ﴿٤ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ ﴿٥ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ ﴿٦
Qul a'uudhu birabbin naas. malikin naas. ilaahin naas. minsharril was-waasil khannaas. alladhii yuwaswisu fiiswuduurin naas. minaljinnati wan naas  mara 3 asubuhi na wakati wa kulala
hizi tatu za mwisho utapulizia kwenye viganja vyako wakati unasoma au baada yake kisha jifute mwili mzima.*
أعوذ بكلمات الله التامات من شر ما خلق 
A'uudhu bikalimaati llaahit taammaati minsharri maa khalaqa.  mara 3 baada ya maghribi
 بسم الله الذي لا يضر مع اسمه شيء في الأرض ولا في السماء وهو السميع العليم،
Bismillaahi lladhiy laa yadhwurru ma'asmihii shai-un fil-ardhwi walaa fis samaa-i wahuwas samii'ul-'aliim.  mara 3 asubuhi na jioni.

In shaa Allah ukiwa na swali au jambo lolote wasiliana nami kwa namba  0715604488