ASALI NA HABAT SAUDAA DHIDI YA UGUMBA.

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته.
Amesema Allah mtukufu kuhusu Asali pale alipo wazungumzia nyuki.
يَخْرُجُ مِنْ بُطُونِهَا شَرَابٌ مُخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِلنَّاسِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
Na kutoka matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbali mbali; ndani yake kina matibabu kwa wanaadamu. Hakika katika haya ipo Ishara kwa watu wanao fikiri.
(Annahli -69).
Ameizungumzi Mjumbe wa Allah Swalla Llaahu alayhi wasallama kufaa kwake Habbat Saudaa.
عن أبي هريرة -رضي الله عنه- أنه سمع رسول الله -صلى الله عليه وسلم- يقول: »في الحبة السوداء شفاء من كل داء، السام( رواه البخاري،5688)
Amesimulia Abuu Hurairah Allah amridhie,Hakika amemsikia Mtume wa Allah
 صلى الله عليه وسلم anasema,kuhusu Habbat Saudaa ni dawa ya kila ugonjwa (Bukhariy 5688).
Ugumba ni hali ya Mwanamke kutopata ujauzito, Mwanaume pia aweza kuwa mgumba
.

Yawezekana Mwanamke asishike mimba kabisa,au
ashike lakini zinaharibika,ikiwa tatizo laweza kutibika Hospitalini atatibiwa na atapona kwa matakwa ya Allah mtukufu.
Mara nyingine yaweza kuwa kuna Jini amemkalia katika fuko la uzazi kila mimba ikikaa anaiporomosha,au anaiacha ikue kidogo kisha anaiporomosha.
Dalili ya kutoka mimba kwa ajili ya Shetani wa Kijini ni kuwa utokaji wake ni wenye kufanana,mathalan akiota ndoto fulani akiamka maumivu yameanza na mwishowe ni mimba kutoka.
Tiba yake.
(1)Asomewe aya za Ruqya,au asikilize kila siku asubuhi na jioni.
(2)Asome surat Aswaaffaat kila siku asubuhi au asikilize.
(3)Asome suratul Maarij kila siku wakati wa kulala.
(4)Yasomewe mafuta ya Habat Saudaa.
(a)Suratul Faatiha.
(b) Aayatu Kursiyu.
(c)Suratul Baqarah aya 284-256.
(d)Aali lmraan aya. 189-200.
Apake kabla ya kulala kifuani,paji la uso,na uti wa. mgongo.
Asali nayo isomewe kisomo hicho hicho cha kifungu namba (4) na atakula kijiko cha cha chakula kila siku asubuhi kabla ya kula chochote.
Matibabu haya yafanyike ndani ya mwezi mmoja,biidhni Llahi atapata mtoto,wamefanyiwa wengi na wamefanikiwa,ama kuhusu Mwanaume tulitoa somo lake matoleo yaliyopita.
Pamoja na hayo muhusika ajitahidi kumuelekea Allah kwa maombi,hakika yeye ndiye ufumbuzi juu ya kila jambo.
Imetolewa na.
Abuu Imraan.
Said Khamis Mkama.
0715913480