KUMUUNGUZA SHETANI KWA KUTUMIA QUR'AN

Ndugu Msomaji 
Assalaamu alaykum
kwanza tumshukuru Mungu kwa kutupatia furasa nyingie kwa kuwa hai ktika muda huu na kuweza kuendelea na majukumu yetu ya kila siku.



Leo nimeona nilete somo litakaloweza kumsaidia msomaji wangu mwenye ujuzi wa kusoma Qur'an anapotaka kumsaidia mgonjwa anayesumbuliwa na shetani mkaidi katika mwili wake somo la namna ya Kumuunguza shetani kwa kutumia Qur'an.

Izingatiwe kuwa kabla kuchukua hatua hii unapaswa kupitia hatua za kumlingania shetani aache vitendo anavyofanya vya kukaa / kumtesa mja huyo wa Mwenyezi Mungu na kwamba vitendo hivyo ni dhulma na Mungu anavichukia utamlingania atoke humo na ajiunge na majini wanaofanya ibada unafanya haya yote huku ukimtolea dalili (ushahidi) wa unachomueleza kutoka katika Qur'an na Sunnah.

Angalizo: Wewe unayemsomea Qur'an unapaswa kuwa mtu safi kwa maana ya ibada hazikupiti na pia mwenye kujiepusha na vitendo na maneno ya kipuuzi unapaswa kuwa ni mwenye kudumu na Adhkaar na dua mbalimbali za kinga, kwa sababu usipokuwa katika hali hizi utakuwa kwenye hatari kubwa ya kushambuliwa na mashetani hayo na pia visomo vyako havitakuwa na matokeo chanya/Mafanikio.

Njia ya kwanza:

Njia hii imegawanyika sehemu tatu:-


  1. Mgonjwa atasomewa/atasikiliza Suratul Baqara yote mara tatu mfululizo katika kikao kimoja.
  2. Mgonjwa atasomewa/atasikiliza Qur'an yote kuanzia Alhamdu mpaka suuratun Naas
  3. Mgonjwa atasomewa/ atasikiliza Yaasin na Suratul Jinn kwa muda wa wiki mbili mfululizo.

ZINGATIA: 

  1. Ni Muhimu kukawepo mtu wa kutoa msaada utakaohitajika kwa mtu atakayekuwa anasikiliza mwenyewe, 
  2. Ni lazima mtu huyo anayesikiliza mwenyewe ama kusomewa awe katika vazi la stara ikiwa mtu huyo ni mwanamke anatakiwa ajifunike mwili mzima ispokuwa uso na viganja vya mikono,ikiwa ni mwanamume ahakikishe kitovu na magoti vimefunikwa kabisa na nguo/ visionekane. 
  3. Awe na udhu,kusiwe na sauti nyinginezo wakati wa kisomo, 
  4. Asikatishe kisomo mpaka kitakapomalizika.
Ndugu msomaji tukutane sehemu ya pili ya somo hili, ikumbukwe kuwa tunafanya juhuzi hizi ili kuwaondoa watu wasitumie njia za kishirikina katika kutatua shida zao mbalimbali ambazo mara nyingi husababisha hasara kwa taifa ikiwemo ukatili na mauji dhidi ya watu mbalimbali. wasiliana nami kwa simu namba 0715604488