KINGA MADHUBUTI DHIDI YA SHARI ZA VIUMBE WOTE-01

Kwanza kabisa nitumie fursa hii ya kuwa hai kumshukuru Mwenyezi Mungu Ambaye hafanani na yeyote wala chochote Kwa kutuwezesha mimi na wewe kuwa hai muda huu kwani kuna wenzetu wengi wapo kwenye maandalizi ya kuhifadhiwa kwenye mochwari,Makaburini na huku wengine wakiwa bado hawajapatikana kutokana na kufa maji, kufa moto ama kuliwa na wanyama porini, sio kwa ujanja wetu bali kwa rehma zake, namuomba Allah awarehemu hao wote waliotangulia pia namuomba awaponye wale wanaougua wakiwa katika hali mbaya muda huu kwani yeye ni muweza wa kila jambo ikiwemo kuwaponya waliokata/waliokatiwa tamaa.

Pia tunaomba mchango wako ili utuwezeshe kutoa kitabu cha dua za tiba na kinga ambacho kimesheheni shuhuda na mawaidha mbalimbali ni kitabu kitakachowasaidia, kuwaelimisha watu wengi zaidi, Toa sadaka yako sasa na wewe uingie katika watakaopata thawabu za watakaoongoka kutoka katika ushirikina na maovu mbalimbali, gharama za uchapaji wa kitabu ni kubwa hivyo msaada wako ni muhimu tuchangie kwa njia zifuatazo:-  
TIGO PESA No. 0715604488 M-PESA No. 0758293138 
kwa wale wasomaji wetu wa nje ya nchi wawasiliane nami kwa simu na whatsapp namba +255715604488

Ndugu Msomaji,
Leo nimependelea kukuletea mafundisho haya ya kuzijua kinga madhubuti dhidi ya shari za viumbe wote kwa idhini ya Allah ili iwe ni sadaka yangu kwako ikuwezeshe kujilinda dhidi ya viumbe wote, kama nilivyo tangulia kueleza katika masomo yangu huko nyuma kuwa Uislam ni mfumo kamili wa maisha ya binaadamu hivyo haitatokea binaadamu akawa na hitajio katika maisha halafu likakosekana ndani ya uislam.

Nakuletea mafundisho haya ili uyatumie badala ya kuhangaika kwa waganga wakakuchanja mwilini eti ndio wanakukinga hapana chukua hii kwani ndio kinga ya kisharia ambayo kwa kuitumia unapata thawabu na ulinzi pia, kuliko kwenye ushirikina unakosa vyote hupati ulinzi wowote lakini pia unapata dhambi kwa kujikinga kishirikina kwa kutatufuta ulinzi pia ni ibada haitakiwi kuelekezwa kwa yeyote ispokuwa Mungu Muumbaji,  Ufuatao ni mfululizo wa kinga hizo:-

Kinga No.1
Kula Tende

Kula tende mbivu saba kila siku kama anavyosema Mtume Muhammad Swalla llaahu alayhi wasallam:- 



Kinga No.2
Kuwa Na Udhu

Uchawi haumuathiri Muislamu mwenye udhu, kwani Muislam Mwenye udhu hulindwa na Malaika wa Mwenyezi Mungu, Ibni Abbas anasimulia kuwa Mtume Swalla llaahu alayhi Wasallam amesema:-

Kinga No.3

Kudumu Katika Swala za Fardhi kwa Jamaa

Kudumu katika swala za fardhi tena kwa jamaa huwa kunamuweka Muislamu katika amani dhidi ya shari za shetani.

Kinga No.4
Kisimamo Cha Usiku

Anayetaka Kuikinga nafsi yake dhidi ya uchawi basi ajitahidi katika kisimamo cha usiku.

Kwa Mahitaji Ya Visomo vya tiba dhidi ya Maradhi ya Kila aina na visomo vya kufukuza mashetani kwenye Majumba,Maofisi, Mashamba,Magari Au visomo kwa ajili ya Mahitaji Mbalimbali wasiliana nami kwa namba 0715604488 tutakufikia Popote ulipo In shaa Allah.