MADHARA YA ZINAA DUNIANI NA AKHERA-02
MTUME (S.A.W) AONYA KUHUSU ZINAATumeona somo lililopita jinsi Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyo ikataza zinaa hata kwa kuisogelea tu, sasa hivi tunaingia kwa Mtume wetu Muhammad (S.A.W) naye amesema mengi juu ya hiyo zinaa, na hakusema bure tu.bali kutahadharisha umma kutokana na yale yatakayowafikia kutokana na madhara ya zinaa.
Kutokana na Mama Aisha (R.A) Amesema, Mtume (S.A.W) Amesema
"Enyi umati Muhammad la mungelijua yale ninayo yajua mimi basi mungali cheka kidogo na mungali lia sana".
(Bukhari na Muslimu)
Nani anaweza kuyapinga maneno haya? Kila Mzinifu hujiona yumo katika starehe kupita kiasi, moyo wake hujawa na furaha akutanapo na mzinifu mwenziye, Vicheko na tabasamu hutawala hapo, nini utamwambia akakuelewa, zaidi ya kukucheka na kukuona mshamba uliyepitwa na wakati, kama angali jua yanayo msubiri mbele yake kuanzia duniani na Akhera basi angali cheka kidogo na angali lia sana.
Je Mzinifu tumuhesabu ni Muumini?
Kutokana na Abuu Hurairah (R.A) amesema . Mtume (S.A.W) amesema
"hazini mzinifu wakati anazini akawa ni Muumini"
(Bukhari na Muslimu)
Hayo ni Duniani je huko akhera na siku ya kiama mzinifu atakuwa katika hali gani?
Kutokana na Abii Hurairah (R.A) amesema. Mtume (S.A.W) amesema,
"watu wa namna tatu hawato semeshwa na Mwenyezi Mungu siku ya kiama, Na hatowatakasa, Na hatowaangalia nao ni juu yao adhabu iumizayo, Mtu mzima mzinifu,Mfalme Muongo na Maskini mwenye kiburi".
(Muslimu)
Yawezekana Kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu akataze jambo bila kujua madhara yake?
Kutokana na Abii Bakrata (R.A) amesema, Mtume (S.A.W) amesema,
"Hakuna Dhambi anayozalisha haraka Mfanyaji wake kwa Kwa Mwenyezi Mungu Mateso duniani na inayokusanya ya Akhera kama Umalaya".
(Ibun Majaha 4211, Tirmidhi 25 na Ameisahihisha Sheikh Alban Kwenye Sahihi yake917)
Ndiyo Mtume (S.A.W) akasema kwa kuogopea zinaa mashaka yake hapa duniani na Akhera.
Kutokana na Abdillahi Ibnu Zaid ( R.A) amesema nimemsikia Mtume (S.A.W) anasema
"hakika hofu ninayo hofia kwenu ni zinaa".
(Tabran na amesema ni hadithi Hasan Sheikh Alban katika Sahihi yake 917)
Itaendelea........
Unaweza kukipata kitabu hiki kwenye maduka yote ya vitabu vya kiislam nchini, kumbuka kuwa kinaitwa MADHARA YA ZINAA DUNIANI NA AKHERA.