MADHARA YA ZINAA
DUNIANI NA AKHERA-01
Msomaji Mpendwa
Assalaamu Alaykum
Leo Katika Kuendeleza Juhudi Zetu Katika Kuuelimisha Umma huu Juu ya Mambo Mbali Mbali Ili yaweze kuwanufaisha katika dunia na akhera Na hatimaye tuweze kuishi katika amani,upendo na umoja miongoni mwetu huku tukiwa na radhi ya Mwenyezi Mungu, Kwa Kushirikiana na Mwandishi Mahiri Wa Vitabu Vya Kiislam Ustadh Said Khamis Mkama Nitawaletea Somo hili Madhara Ya Zinaa Duniani Na Akhera Somo ambalo limebeba pia jina la kitabu hicho , Kitabu hiki unaweza kukipata kwenye maduka yote ya vitabu Vya Kiislam Nchini,
NB nimeweka namba 01 ili kumrahisishia msomaji kufuatilia mfululizo wake. Twende Pamoja.......
MWENYEZIMUNGU (SW) AONYA KUHUSU ZINAA
Enyi Ndugu Zangu Katika Imani, Hakika miongoni mwa madhambi makubwa na misiba ambayo inamuharibia mwanadamu dunia yake na akhera yake, na kumletea huzuni na majuto na masikitiko katika uhai wake wa dunia, na siku watakayosimama watu mbele ya Bwana wa walimwengu wote, ni hili janga la zinaa.
Muonekano Wa Kitabu , Kitabu Hiki Na Vinginevyo
unaweza kuvipata Maduka yote Ya Vitabu Vya Kiislam Nchini
Mwenyezi Mungu Mtukufu ameiharamisha zinaa na akaitahadharisha kwa ukubwa wa tahadhari na akaweka wazi ubaya wake kwa ukubwa wa kuweka wazi kwa kusema.
وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلزِّنَىٰٓۖ إِنَّهُ ۥ كَانَ فَـٰحِشَةً۬ وَسَآءَ سَبِيلاً۬ (٣٢
WALAMUSIIKARIBIE ZINAA HAKIKA HUO NI UCHAFU NA NJIA MBAYA (AL-ISRAAI-32)
Ameiweka sawa katika adhabu Allah Mtukufu, zinaa,shirki na kuua nafsi kwa dhulma, kwa kuahidi adhabu mara mbili kwa mtendaji wake aliposema.
وَٱلَّذِينَ لَا يَدۡعُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ وَلَا يَقۡتُلُونَ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِى حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَلَا يَزۡنُونَۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٲلِكَ يَلۡقَ أَثَامً۬ا (٦٨) يُضَـٰعَفۡ لَهُ ٱلۡعَذَابُ يَوۡمَ ٱلۡقِيَـٰمَةِ وَيَخۡلُدۡ فِيهِۦ مُهَانًا (٦٩
NA WALE WASIO OMBA MUNGU MWINGINE PAMOJA NA MWENYEZI MUNGU, WALA HAWAUI NAFSI ALIYOIHARAMISHA MWENYEZI MUNGU ISPOKUWA KWA HAKI WALA HAWAZINI NA ATAKAYEFANYA HIVYO ATAPATA MADHARA,ATAZIDISHIWA ADHABU SIKU YA KIAMA NA ATADUMU HUMO KWA KUFEDHEHEKA. (ALFURQAAN 68-69)
Aya ya kwanza Mwenyezi Mungu amekataza kuikaribia zinaa kwa maana ya kujiepusha na yale yanayo sababisha mja kuzini,na akabainisha ni uchafu hiyo zinaa, na wala siyo ustaarabu kama wanavyo dhania wengi, na aya ya pili akajumuisha zinaa na madhambi makubwa kama shirki na kuua nafsi ya mtu kwa dhulma, na akaahidi kwa wenye kufanya hayo kupata adhabu ya ziada na kufedheheka.
Hapana shaka maonyo yote ya zinaa yame dhihirika na uhatari wake umeonekana katika jamii, Mwenye akili hasubiri kuambiwa anajionea mwenyewe namna zinaa ilivyosambaratisha ulimwengu. In Shaa Allah huko mbeleni tutaelezea nukta kwa nukta ili wazinduke walio lala. Itaendelea.....