KINGA
MADHUBUTI DHIDI YA SHARI ZA VIUMBE WOTE-01
Kwanza kabisa nitumie fursa hii
ya kuwa hai kumshukuru Mwenyezi Mungu Ambaye hafanani na yeyote wala chochote Kwa
kutuwezesha mimi na wewe kuwa hai muda huu kwani kuna wenzetu wengi wapo kwenye maandalizi
ya kuhifadhiwa kwenye mochwari,Makaburini na huku wengine wakiwa bado
hawajapatikana kutokana na kufa maji, kufa moto ama kuliwa na wanyama porini,
sio kwa ujanja wetu bali kwa rehma zake, namuomba Allah awarehemu hao wote
waliotangulia pia namuomba awaponye wale wanaougua wakiwa katika hali mbaya
muda huu kwani yeye ni muweza wa kila jambo ikiwemo kuwaponya
waliokata/waliokatiwa tamaa.
Pia tunaomba mchango wako ili utuwezeshe kutoa kitabu cha dua za tiba na kinga ambacho kimesheheni shuhuda na mawaidha mbalimbali ni kitabu kitakachowasaidia, kuwaelimisha watu wengi zaidi, Toa sadaka yako sasa na wewe uingie katika watakaopata thawabu za watakaoongoka kutoka katika ushirikina na maovu mbalimbali, gharama za uchapaji wa kitabu ni kubwa hivyo msaada wako ni muhimu tuchangie kwa njia zifuatazo:-
TIGO PESA No. 0715604488 M-PESA No. 0758293138
kwa wale wasomaji wetu wa nje ya nchi wawasiliane nami kwa simu na whatsapp namba +255715604488
Ndugu Msomaji,
Leo nimependelea kukuletea
mafundisho haya ya kuzijua kinga madhubuti dhidi ya shari za viumbe wote kwa
idhini ya Allah ili iwe ni sadaka yangu kwako ikuwezeshe kujilinda dhidi ya
viumbe wote, kama nilivyo tangulia kueleza katika masomo yangu huko nyuma kuwa
Uislam ni mfumo kamili wa maisha ya binaadamu hivyo haitatokea binaadamu akawa
na hitajio katika maisha halafu likakosekana ndani ya uislam.
Nakuletea mafundisho haya ili
uyatumie badala ya kuhangaika kwa waganga wakakuchanja mwilini eti ndio
wanakukinga hapana chukua hii kwani ndio kinga ya kisharia ambayo kwa kuitumia
unapata thawabu na ulinzi pia, kuliko kwenye ushirikina unakosa vyote hupati
ulinzi wowote lakini pia unapata dhambi kwa kujikinga kishirikina kwa
kutatufuta ulinzi pia ni ibada haitakiwi kuelekezwa kwa yeyote ispokuwa Mungu
Muumbaji, Ufuatao ni mfululizo wa kinga
hizo:-
Kinga
No.1
Kula Tende
Kula tende mbivu saba kila siku
kama anavyosema Mtume Muhammad Swalla llaahu alayhi wasallam:-
Kinga
No.2
Kuwa Na Udhu
Uchawi haumuathiri Muislamu
mwenye udhu, kwani Muislam Mwenye udhu hulindwa na Malaika wa Mwenyezi Mungu,
Ibni Abbas anasimulia kuwa Mtume Swalla llaahu alayhi Wasallam amesema:-
Kinga No.3
Kudumu Katika Swala za Fardhi kwa Jamaa
Kudumu
katika swala za fardhi tena kwa jamaa huwa kunamuweka Muislamu katika amani
dhidi ya shari za shetani.
Kinga
No.4
Kisimamo Cha Usiku
Anayetaka
Kuikinga nafsi yake dhidi ya uchawi basi ajitahidi katika kisimamo cha usiku.
Kwa Mahitaji Ya Visomo vya tiba dhidi ya Maradhi ya Kila
aina na visomo vya kufukuza mashetani kwenye Majumba,Maofisi, Mashamba,Magari
Au visomo kwa ajili ya Mahitaji Mbalimbali wasiliana nami kwa namba 0715604488
tutakufikia Popote ulipo In shaa Allah.