DUA ZA KUONDOSHA AINA ZOTE ZA DHIKI
 
Msomaji Wangu Mpendwa
Assalaam alaykum
 
Kwanza kabisa hatuna budi kumshukuru Mungu Wa Pekee aliyeumba kila kitu asiyefanana na  yeyote wala chochote kwa kutuwezesha kuwa pamoja tena katika Mtandao Wetu Bora kabisa Wa Tibasahihi tukielimishana mambo mbalimbali yenye kutufaa katika dunia na akhera yetu Pia tumtakie ziada ya Rehma na Amani Mtume Wetu Muhammad S.A.W na Aali zake na Sahaba zake na wote watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya malipo.
 
Karibu tuanze somo letu hili linalohusiana na Dua Za Kuondosha Aina Zote Za Dhiki naamini darsa hili litatusaidia sana katika kukabiliana na dhiki za aina zote zinazotukabili katika maisha yetu ya kila siku badala ya kukimbilia kwenye ushirikina na uvunjifu mwingine wa Amani.
 
 
Ndugu Msomaji Uislam ni mfumo kamili wa maisha unaowawezesha wanaoufuata kumudu kila jambo linalowakabili na iwe ni katika furaha na hata huzuni na bila shaka dhiki (ugumu wa hali) kimaisha ni katika mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa katika kusababisha huzuni kwa muhusika.
 
Uislam umetufundisha namna ya kukabiliana na hali hiyo na nyinginezo na hapa chini ni miongoni mwa namna hizo. nazo zinatakiwa kusomwa kwa kurudiwa mara nyingi asubuhi na jioni huku msomaji akiwa ana udhu na ameelekea Qibla, zoezi hili unapswa kulitekeleza kwa mfululizo na usiache na kukata tamaa pia wakati unaendelea na zoezi hili huku ukiendelea na kibarua ama biashara zakob hakika Allaah ataweka Baraka zake na hali itabadilika Inshaa Allaah.
 
 
وَٱللَّهُ يُؤۡتِى مُلۡڪَهُ ۥ مَن يَشَآءُ‌ۚ وَٱللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ۬ (٢٤٧)
 
وَٱللَّهُ يُضَـٰعِفُ لِمَن يَشَآءُ‌ۗ وَٱللَّهُ وَٲسِعٌ عَلِيمٌ (٢٦١)
 
قُلۡ إِنَّ ٱلۡفَضۡلَ بِيَدِ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُ‌ۗ وَٱللَّهُ وَٲسِعٌ عَلِيمٌ۬ (٧٣)
 
ذَٲلِكَ فَضۡلُ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُ‌ۚ وَٱللَّهُ وَٲسِعٌ عَلِيمٌ (٥٤)
 
إِن يَكُونُواْ فُقَرَآءَ يُغۡنِهِمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦ‌ۗ وَٱللَّهُ وَٲسِعٌ عَلِيمٌ۬ (٣٢)
 
 وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَىۡءٍ عِلۡمًا‌ۚ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡنَا‌ۚ رَبَّنَا ٱفۡتَحۡ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَ قَوۡمِنَا بِٱلۡحَقِّ وَأَنتَ خَيۡرُ
ٱلۡفَـٰتِحِينَ (٨٩)
 
وَرَحۡمَتِى وَسِعَتۡ كُلَّ شَىۡءٍ۬‌ۚ فَسَأَكۡتُبُہَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّڪَوٰةَ وَٱلَّذِينَ هُم بِـَٔايَـٰتِنَا يُؤۡمِنُونَ (١٥٦)
 
إِنَّمَآ إِلَـٰهُكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِى لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ‌ۚ وَسِعَ ڪُلَّ شَىۡءٍ عِلۡمً۬ا (٩٨)
 
 رَبَّنَا وَسِعۡتَ ڪُلَّ شَىۡءٍ۬ رَّحۡمَةً۬ وَعِلۡمً۬ا فَٱغۡفِرۡ لِلَّذِينَ تَابُواْ وَٱتَّبَعُواْ سَبِيلَكَ وَقِهِمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ (٧)
 
 
 
Pia unaweza kusoma dua hii mara 7
 
‏  لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ الْعَظِيمُ الْحَلِيمُ، لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ رَبُّ السَّمَوَاتِ، وَرَبُّ الأَرْضِ، وَرَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ
 
 
 
SHUKRANI ZA DHATI KWAKO DADA SAUMU
 
Mwisho nichukue fursa hii kumshukuru na kumuombea Dua Dada yangu Mpendwa na Mumewe kwa wema na ukarimu mkubwa walionifanyia kwa kunifadhili kitendea kazi Laptop Mpya kabisa  huku tukiwa na muda mfupi tu tangu tuanze kuwasiliana na kuanza taratibu za visomo hakika namuomba Allaah awabaarik kwani sasa kazi yangu ya Uandishi imekuwa nyepesi sana ukilinganisha na hapo  kabla kwani nilikuwa natumia Internet Café

namuomba Allaah ajaalie thawabu za da'wa hii ziwafikie na wao na wengine watakaojitolea kuuwezesha mtandao huu kufikisha ujumbe wa Allah sehemu mbalimbali za dunia kwani Alhamdulillah Mpaka sasa kwa rehma za Allah tumeweza kuzifikia takribani nchi 46 , pia natoa wito kwa  wasomaji wangu wengine wenye kutarajia malipo kwa Allaah na watakaopenda kushiriki katika sadaka hii wawasiliane nami kwani bado nina mapungufu kadhaa katika vitendea kazi nanyi pia Allaah atawalipa.
 
 
 
 
 
Mpendwa Msomaji wangu ukiwa na swali,ushauri au maoni  nifuatilie kupitia twitter kwa kuponyeza hapa https://twitter.com/HemediPalike