MAUAJI HAYA DHIDI YA ALBINO YAKOMESHWE
Msomaji Wangu Mpendwa
Assalaamu alaykum,
Katika Miaka ya Hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia kukithiri kwa vitendo vya kikatili dhidi ya Watanzania wenzetu wenye ulemavu wa Ngozi Albino
Tumekuwa tukishuhudia na kusikia kuuawa kwa Watanzania hawa dhaifu huku wengine wakiachwa wakiwa hawana baadhi ya sehemu za viungo vyao, imekuwa ikionekana kama ni kawaida kusikia sehemu fulani ima ameuawa Albino ama amekatwa kiungo/viungo.
Kimsingi vitendo hivi havikubaliki hata kidogo kwani Mwenyezimungu ameharamisha mauaji yoyote yaliyo kinyume na sheria
Hapo utaona Mwenyezimungu Muumba wa majini na watu anakemea kuua nafsi (mtu) pasi na haki (sababu kama vile ikiwa mtu huyo imethibitika kuwa ameua hapo na yeye itakuwa ni halali kuuawa) sasa hawa ndugu zetu Albino wananyanyaswa kwa sababu ya unyonge na uchache wao au kipi kinachowapa kiburi na ujasiri wauaji hawa?
SABABU KUU YA MAUAJI HAYA NI USHIRIKINA
Walemavu wa Ngozi mara nyingi huuawa ama kukatwa viungo vyao, Makatili hawa ambao ni zaidi ya wanyama hutekeleza unyama wao huu kwa kisingizio tena baada ya kudanganywa na waganga washirikina kuwa viungo wa Albino vinaweza kuwatajirisha kitu ambacho ni uwongo ulio dhahiri,
Hakuna kiungo cha binadamu yeyote kinachoweza kuwa sababu ya kupata utajiri tuacheni uvivu tujitume ili tuweze kuwa na taifa lenye ucumi imara lililobarikiwa na Mwenyezimungu kwani vitendo Hivi vinaathiri kwa kiwango kikubwa uchumi na nguvu kazi ya taifa,
Unapomkata mkono au mguu Mlemavu wa ngozi unachangia kwa kiasi kikubwa kumtia umasikini yeye binafsi na wategemezi wake na hivyo kulisababishia taifa hasara ya kupungukiwa na wazalishaji mali, katika ulimwengu huu tunaoishi ajira ni ngumu zaidi kwa walemavu waajiri wamekuwa wagumu mno kutoa nafasi kwa watu wenye ulemavu natoa wito kwa watanzania wenzangu wapenda amani kushikamana kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika na usalama za nchi yetu Katika kupambana na hatimaye kutokomeza vitendo Hivi visivyo vya kibinadamu.

PENDEKEZO LANGU KWA MAMLAKA HUSIKA.
Hakuna namna ya kusalimika na kukomesha mauaji haya ispokuwa ni kutekeleza hukumu ya kifo kwa wauaji hawa tena ikibidi yawe ya hadharani ili iwe fundisho na kemeo kwa wengine wenye tamaa ya utajiri ama madaraka iwe mtu huyo aliyekamatwa kwa mauaji ametumwa au muhusika mkuu ni yeye mwenyewe wote aliyetumwa na aliyetuma wote hukumu ya kifo itekelezwe dhidi yao.
Haiwezekani tuwe na taifa salama huku tukiacha Watanzania wenzetu wakiuliwa kwa dhulma tusikubaliane na maneno ya watu wanaodai na kutetea kuwa eti wauaji nao wana haki ya kuishi
Mwenyezimungu anasema kwenye kitabu chake cha Qur'aan
Kwani Muuaji akiuawa inakuwa kemeo halisi kwa mwingine mwenye tabia chafub kama hiyo maana atajua fika kuwa ikithibitika ameua na yeye atauawa.
Nawakilisha hoja yangu na pendekezo langu kwenu watanzania wenzangu na ninawapenda nyote.
"ALBINO NAO WANA HAKI SAWA YA KUISHI TENA WAKIWA NA VIUNGO VYOTE VYA MWILI, EPUKA NA SHIRIKI KUEPUSHA UKATILI DHIDI YAO". Mpendwa Msomaji wangu ili kupata haya na mengineyo nifuatilie kupitia twitter kwa kuponyeza hapa https://twitter.com/HemediPalike