FUNGA YA RAMADHANI NA  MAELEKEZO YAKE-01

Maelezo ya Swaumu Na Kufaradhishwa Kwake  

1.    Maelezo ya Swaumu
 
Swaumu Kilugha:Ni kujizuilia. Kisheria: Pamoja na nia ya kufanya ibada na kula na kunywa Na kujiepusha kutazama wanawake kwa matamanio na yenye kufunguza tangu kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuchwa kwa jua.

2.    Tarehe ya Kufaradhishwa Swaumu

Mwenyezi Mungu Mtukufu
alifaradhisha swaumu juu ya ummati wa Muhammad s.a.w kama alivyofaradhisha juu ya umma zilizotangulia kwa kauli yake Allah Mtukufu:

 

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡڪُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِڪُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ 

 



“Enyi ambao mlioamini mmefaradhishiwa funga kama walivyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu”
Albaqara :183

 

Na hiyo ilikuwa siku ya jumatatu ya mwezi wa sha’abaan mwaka wa pili wa hijra iliyobarikiwa.
 
Wasomaji wangu Wapendwa Tukiwa kwenye kipindi cha Maandalizi ya Mwisho katika kuuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Na Zikiwa zimebakia takriban siku 28, Na mimi nikiwa miongoni mwa waumini ambao kama Allaah atapenda niwemo miongoni mwa wafungaji kwa maana ya kuwa hai na afya na kuwafikishwa kufunga nimeonelea niwaletee mfululizo huu wa mafundisho yahusuyo Swaumu Nami iwe sadaka yangu Kwa Kila atakayesoma tuonane sehemu 2 ya Somo hili ambalo In Shaa Allah litakuwa linakujia Mara 3 kwa wiki .


Pia kwa atakayependa Kupata vitabu vyenye mafundisho mbalimbali kuhusu dini ya Kiislamu ikiwemo Swaumu basi namshauri awatafute
 IBN HAZM MEDIA CENTER Ambao wanapatikana Msikiti wa Mtoro Kariakoo, Dar Es Salaam Hapo wataweza kupata Vitabu Vyote Vya Elimu ya Kiislam Kama Vile FIQH,SIRA,BALAGH,LUGHA N.K Pia vinapatikana vitabu Mbali Mbali vilivyotafsiriwa katika lugha ya Kiswahili na JOPO LA WANAVYUONI WA KIISLAM.