SHETANI ANASILIMU NA KUMTAPISHA
UCHAWI MGONJWA BAADA YA KUSOMEWA RUQYAH
Ndugu Msomaji
Assalaamu alaykum,
Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba Wa Mbingu Na ardhi na vilivyomo ndani yake na baina yake kwa kuuweze kukutana tena hapa kwenye mtandao wetu tunaoutumia kuelimishana mambo mbalimbali yanayotuwezesha kufahamu namna halali za kujitibu/kutibiwa bila ya kushiriki katika tiba za kishirikina.
Pia tunaomba mchango wako ili utuwezeshe kutoa kitabu cha dua za tiba na kinga ambacho kimesheheni shuhuda na mawaidha mbalimbali ni kitabu kitakachowasaidia, kuwaelimisha watu wengi zaidi, Toa sadaka yako sasa na wewe uingie katika watakaopata thawabu za watakaoongoka kutoka katika ushirikina na maovu mbalimbali, gharama za uchapaji wa kitabu ni kubwa hivyo msaada wako ni muhimu tuchangie kwa njia zifuatazo:-
TIGO PESA No. 0715604488 M-PESA No. 0758293138
kwa wale wasomaji wetu wa nje ya nchi wawasiliane nami kwa simu na whatsapp namba +255715604488
Leo nimeona niwafafanulie wasomaji wangu mambo machache
kuhusu mashetani (mapepo) kwani watu wengi wamekuwa na uelewa mdogo kuhusu
viumbe hawa.
Ukweli ni kwamba majini ni viumbe miongoni mwa viumbe wa
mwenyezimungu kama Qur'aan inavyotueleza
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا
لِيَعْبُدُونِ
"sikuumba majini na watu illa waniabudu"
Adhariayaati:56
hapo tunapata ushahidi kuwa majini na wanaadamu wameumbwa na
Allaah kwa ajili ya ...ibada tu. na sio kuwafanya wanadamu kuwa viti vyao maana mara nyingi binadamu mwenye shetani huitwa kiti, hupelekeshwa na shetani huyo kwa mambo mbalimbali.
na baada ya kuasi majini na wanaadamu ndio wakaitwa
mashetani lakini maarufu kwa jina hilo la mashetani ni majini.
pia ni vyema tukatambua kuwa wapo majini wema kama
walivyokuwepo wanaadamu wema na pia wapo majini waovu mfano wa wanaadamu
vilevile.
Itambulike kuwa wapo majini waislamu,wakristo tena walokole,
mayahudi,pia wapo wanaojitambulisha kwa makabila mbalimbali
nimepata kumlingania jinni wa kilokole na nilimtambua baada
ya kupanda kichwani kwa mgonjwa na kuanza kunikemea kama wafanyavyo walokole,
Hii ilikuwa mwaka 2010 nilifuatwa na mmoja wa majirani zangu
na kunishitakia tatizo la binti yake aliyekuwa anashindwa kwenda shule kwa
sababu ya mashetani wakati huo akiwa kidato cha nne!
Siku ya kwanza nilipoelezwa matatizo ya binti huyo ilikuwa
alhamisi sikumbuki tarehe lakini ilikuwa mwezi april,niliishia kuyasomea maji
kisomo cha Ruqyah kisha nikawaaga na kuondoka kwakuwa nilikuwa nahitajika kwa
mgonjwa mwengine aliyekuwa na hali ngumu zaidi kwa muda huo.
Nyuma yangu kumbe kulitokea matatizo mazito kiasi cha kusababisha
mgonjwa kufungwa mikono na miguu niliyafahamu haya baada ya kurudi siku ya pili
baada ya swala ya ijumaa,
Siku hiyo wakachukua namba zangu za simu lipofika saa 11:30
jioni wakanipigia simu kuwa hali ni mbaya kwakuwa sikuwa mbali na kwao nikarudi
na kumkuta mgonjwa hana fahamu.
Nikaanza kumsomea kisomo cha Ruqyah baada ya muda shetani
akapanda nikamlingania kuachana na dhulma alidai hana dini nikamlingania juu ya
uislamu akanielewa ALHAMDU LILLAAH akasilimu na akaondoka, mara akapanda
mwingine wa kike akaanza kufanya dhihaka mbalimbali lakini kwa kuwa nimejaaliwa
kufahamu sehemu ya vitimbi vyao sikujali nilipoendelea na kisomo akaanza vituko
vyake akiniambia ushindwe katika jina la yesu nami nikamuambia utashindwa wewe
katika jina la ALLAH.
Ilinichukua muda mrefu wa kisomo ndipo kibao
kilipombadilikia na kuanza majuto akimtaja yesu kwamba amemdanganya!
nikamwambia sio kweli nikamueleza ukweli aliokuja nao yesu na jinsi
ulivyopindishwa!
Kumbe Kabla Alikuwa Muislam!
Kumbe aliwahi kuwa muislamu akadanganywa na shetani mkristo
akartadi,kwakuwa yule mgonjwa alikuwa akilalamikia maumivu ya kifua nilimuamuru
yule shetani autoe uchawi wake akasema atakuja kuutoa mumewe (shetani wa
kiume)kwani ndiye aliye uweka.
nikamlimngania uislamu akaukubali LILLAHIL HAMDU na yeye
akasilimu,muda wa swala ya maghribi ulikuwa umeshafika tukaenda kuswali,
Tuliporudi nikaanza kusome dua kwa ajili ya kumuomba ALLAH
alikinge eneo husika baada ya kuondoa picha zote za viumbe ahai ndani awali
sikulizingatia hilo la kutoa mapicha kwa kuwa hali ya mgonjwa haikuwa nzuri
nikafanya Ruqya katika hali ya dharula (
lakini kuepusha mapicha,miziki n.k ni lazima kabla ya kisomo kwani malaika
hawaingiii kwenye nyumba yenye picha za viumbe hai…)
kabla sijamaliza kusoma dua shetani akapanda kwa mgonjwa na
kisomo kiliendelea kwa muda mrefu sana mwisho ALLAAH kaleta tawfiq yake kwani
shetani alisalimu amri akakubali kuutoa uchawi aliomlisha mgonjwa na
nilipomuhoji alimlisha wakati gani akasema wakati alipokuwa anakula chipsi
shuleni (siku aliyoanguka mara ya kwanza)
Pia alilinganiwa uislam akasilimu na kutoka baada ya muda
mfupi mgonjwa akarejewa na fahamu zake, nilipomuuliza mimi ni nani akanitaja
jina langu na pia aliwatambua ndugu na wazazi wake,
nilipomuuliza kuhusu maumivu aliyokuwa anayalalamikia
akajibu kuwa hayasikii tena! ALHAMDU LILLAAH kwani Munug ndie aliyeyatenda yote
mimi nilikuwa ni sababu tu.
Jumatatu yule binti akaanza kwenda shule kama kawaida,Watu hawa Mwenyezi Mungu alitaka kuwaokoa na shirki kwani walishakwenda kwa
mganga na kutakiwa kuku saba na mbuzi wawili,
KAMA UNAHITAJI KUSOMEWA DUA PIGA SIMU
NAMBA +255715604488
NB:sina nia ya kuwakejeli watu kwa imani yao, kwani baadae
inshaa ALLAH nitawaeleza pia kuhusu majini waislamu niliopata kuwalingania kwa
wagonjwa na vituko vyao.
HUDUMA HII INAPATIKANA KWA WATU WOTE BILA KUBAGUA DINI YA
MTU PIA TUNA HUDUMIA WANAOISHI NJE YA NCHI NA TANGU TUNAANZA TUMEKUWA TUKIWAHUDUMIA WATU WA ITIKADI ZOTE. NYOTE
MNAKARIBISHWA.