UMUHIMU WA KUOMBEANA DUA

Ndugu Msomaji,
Assalaamu alaykum

Awali ya yote hatuna budi tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kuwa hai katika muda huu na kwa kutujaalia kuwa na afya kwa kiasi hiki, hakika hii tuliyonayo ni neema kubwa sana.

Niingie katika mada yangu niliyoikusudia kukufikishia leo Msomaji wangu Mpendwa kama kilivyo kichwa cha habari hapo juu.

Mtume Muhammad Swalla llaahu alayhi wasallam anasema

وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال‏:‏
 ‏ "‏الدعاء هو العبادة‏"‏‏.‏
"Dua ni Ibada"

Hapa tunajifunza kuwa kufanya maombi ni ibada maana yake tukimuomba Mwenyezi Mungu tunakuwa tunamuabudu na tunapata thawabu kutokana na kitendo hicho, hivyo tukiomba kiumbe{kama vile mzimu,shetani,kaburi n.k} badala ya Kumuomba Muumbaji inakuwa shirki na anayefanya hivyo anapata dhambi.

Ieleweke kuwa dua inaweza kuwa ni kumuomba Allah akupe jambo au kitu fulani au akulinde dhidi ya kitu, Mtu, au kiumbe fulani

KUJIBIWA DUA.

Ndugu Zangu hatukuamrishwa kumuomba Allah tu bali Allah ametuahidi kutujibu Maombi yetu kama alivyosema kwenye kitabu chake cha Qur-an 

 أُجِيبُ دَعۡوَةَ ٱلدَّاعِ إِذَا دَعَانِ‌ۖ
"...Ninajibu Maombi Ya Muombaji Anaponiomba"

hii ni ahadi ya Allah ambayo ni ya uhakika kuwa anayemuomba atarajie kupata majibu ya maombi yake.

KUMUOMBEA ALIYE MBALI.

Na katika hili la kumuombea dua aliyembali Kuna wasomaji wangu kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wakiniuliza kama kuna uwezekano wa kuwaombea dua za kuondoa shida zao mbali mbali nimekuwa niwaelimisha kuwa inawezekana  na
Alhamdulillah wengi wao wameelewa.

Mtume swalla llaahu alayhi wasallam amesema:-

وعنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يقول‏:‏ ‏ "‏دعوة المرء المسلم لأخيه بظهر الغيب مستجابة، عند رأسه ملك موكل كلما دعا لأخيه بخير قال الملك الموكل به‏:‏ آمين، ولك بمثل‏"‏ ‏(‏‏(‏رواه مسلم‏)‏‏)‏‏.


"Dua ya Muislam kwa ndugu yake aliyembali inajibiwa....."

Ndugu zangu ninawausia na kuwahimiza juu ya kuombeana dua kwa shida zetu mbalimbali na pia tujue kuwa wakati tunawaombea wenzetu na sisi pia tunaombewa na Malaika 

Kuna faida nyingi za kuombeana miongoni mwazo ni kuimarisha udugu na upendo miongoni mwetu.

Kuna Wasomaji wangu wengi tu wamekuwa wakinitaka kuwaombea dua nami nawafanyia hivyo miongoni mwao ni Dada yangu (msomaji wangu wa Canada) ana mama yake anasumbuliwa na maradhi kwa muda sasa namuombea kwa Allah ampe subira yeye na wanaomuuguza wawe na msimamo huu huu wa kutofanya ushirikina ili tu Mgonjwa apone, Pia namuombea shifaa(ponyo) la karibu litokalo kwa Allah In shaa Allah. Pia niwaombe wasomaji wangu tushiriki kila mmoja wetu kwa nafasi aliyonayo wakati wowote atakaoisoma post hii asome aya zifuatazo kwa niya ya kumombea mgonjwa huyu na wengineo.

ذٰلِكَ تَخۡفِيۡفٌ مِّنۡ رَّبِّكُمۡ وَرَحۡمَةٌ
Mara 7

 وَيَشۡفِ صُدُوۡرَ قَوۡمٍ مُّؤۡمِنِيۡنَۙ‏
Mara 7

وَاَوۡحٰى رَبُّكَ اِلَى النَّحۡلِ اَنِ اتَّخِذِىۡ مِنَ الۡجِبَالِ بُيُوۡتًا وَّمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُوۡنَۙ‏ ﴿۶۸﴾  ثُمَّ كُلِىۡ مِنۡ كُلِّ الثَّمَرٰتِ فَاسۡلُكِىۡ سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا‌ ؕ يَخۡرُجُ مِنۡۢ بُطُوۡنِهَا شَرَابٌ مُّخۡتَلِفٌ اَلۡوَانُهٗ فِيۡهِ شِفَآءٌ لِّلنَّاسِ‌ؕ اِنَّ فِىۡ ذٰ لِكَ لَاٰيَةً لِّقَوۡمٍ يَّتَفَكَّرُوۡنَ‏ 

Mara 3
وَاِذَا مَرِضۡتُ فَهُوَ يَشۡفِيۡنِ
Mara 7
Unaweza kusoma zote au moja wapo ama kuhusu idadi hilo ni pendekezo langu tu unaweza kusoma zaidi ya idadi hiyoKwa kufanya hivyo utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa mwenzako lakini na kwako binafsi.

Mwisho nichukue fursa hii kuwatahadharisha wanaonipigia simu kutaka huduma za kishirikina, pete za bahati, pesa za majini nawasisitiza mimi sijihusishi na vitu hivyo kwani ni haramu kwa mujibu wa imani yangu, badala yake nakukaribisha kupata  huduma za visomo/ dua kwa ajili ya shida na haja mbalimbali. Nawapenda Nyote kwa Ajili ya Allah.