Soma na Uzingatie Kisa hiki cha
MCHAWI,MTAWA NA KIJANA
Assalaamu Alaykum
Ndugu Msomaji
Kama ilivyo ada awali ya yote
tuchukue fursa hii kumshukuru Allah mola mlezi wa viumbe wote yeye ndie
aliyeumba mbingu na Ardhi na vilivyomo, hafanani na yeyote wala chochote hakika
yeye Allah anasikia kila kitu na anaona kila kitu.
Kisa hiki anakisimulia mtume
Muhammad Swalla llaahu alayhi wasallam kuwa “Alikuwepo katika watu
waliokuwa kabla yenu Mfalme ambae alikuwa na mchawi.
Mchawi Yule alipokuwa mtu
mzima sana kwa uzee wake alimwambia mfalme, “Hakika mimi limekuwa kubwa rika
langu na nimehudhuria ajali yangu, nitafutie kijana nimfundishe uchawi. Mfalme
akampelekea kijana akawa anamfundihs
uchawi na likuwa baina ya mchawi na mfalme mtawa wa kinaswara. Kijana Yule
akaenda kwa Yule mtawa na akasikiliza mafundisho yake ukamvutia ufasaha wake na maneno yake, na
akawa anapomwendea mchawi
anampiga na kumwambia ni jambo gani lililokuchelewesha? Na akiwa anakwenda kwa
watu wake humpiga na kumwambia ni jambo gani liliokuchelewesha? Yule kijana
akaeleza hali yake { ya kupigwa na Yule
mchawi} kwa Yule mtawa, akamwambia
hakika mchawi akikupiga sema
wamenichelewesha watu wangu, na wakitaka watu wako kukupiga sema
amenichelewesha mchawi.
Siku moja katika ada yake ghafla
akiwa anakwenda kwa Yule matawa alitokea
mnyama mkubwa sana amewazuia watu
hawawezi kupita. Kwa kutokea jambo lile akasema leo nitaelewa jambo la mtawa
je, linapendeza sana kwa mwenyezimungu au jambo la mchawi ndio lenye kupendeza?
Amesema, Mara kijana Yule akachukua jiwe
akasema, ‘Ee Mola wangu wa haki likiwa jambo la mtawa linapendeza sana kwako na
linaridhiwa sana kuliko jambo la mchawa basi muue mnyama huyo ili watu waweze
kupita’ akamtupia jiwe mnyama Yule na
akamuua na watu wakapita.
Kijana akamueleza mtawa habari
ile akasema: ‘Ewe kijana change wewe ni
mbora kuliko mimi na utapata majaribio, utakapopatwa na majaribio
usiwafahamishe watu kuhusu mimi, ikawa kazi ya kijana Yule kuwaponesha vipofu, na wenye mbalanga na baki ya
magonjwa.
Mfalme alikuwa ana rafiki katika
baraza lake akapofuka akasikia kuhusu habari ya za kijana Yule akamwendea na
zawadi nyingi sana akamwambia niponyeshe
na utapata wewe vitu vyote nilivyo navyo. Yule kijana akasema Sikuwa mimi
ninamponya mtu yeyote, hakika hapana jambo lolote nifanyalo ispokuwa Mwenyezi
Mungu, mwenye kushinda , mwenye utukufu , ukimwamini nitamwomba na atakuponyyesha,
Yule bwana akaamini – na Yule kijana akamuombea Mwenyezi Mungu na akapona.
Kisha akamwendea Mfalme akakaa
kwake palepale alipokuwa anakaa, Mfalme akamuuliza “Eee Fulani ni nani
aliyekurudishia kuona kwako? Akasema:
“Ni Bwana wangu, akasema: mimi? Akasema: Hapana
Bwana wangu na Bwana wako ni Mwenyezi Mungu.
Mfalme Akasema ,jee wewe una
Bwana asiyekuwa mimi? Akasema: Ndiyo Bwana wangu na Bwana wako ni Mwenyezi
Mungu. Mfalme akawa anamtesa hadi akajulishwa kuhusu kijana Yule, Mfalme
akapeleka ujumbe kwa Yule kijana
akasema” “ Ewe kijana change, umefikia
katika uchawi wako kiasi cha kuwa unawaponyesha vipofu, na wenye mbalanga? Na
magonjwa mengine haya? Yule kijana akasema mimi simponyeshi mtu yeyote hakika
hapana jambo lolote bali anayeponyesha ni Mwenyezi Mungu , Mwenye
Kushinda, Mwenye kutukuka, Mfalme akasema: Ni mimi? Kijana akajibu ‘hapana’
Mfalme akamuuliza ‘Hivi wewe una Bwana
mwingine asiyekuwa mimi? Kijana akasema:
Bwana wako na Bwana wangu ni Mwenyezi Mungu. Mfalme akamuadhibu kijana
Yule kwa adhabu mbali mbali kiasi cha Yule kijana kutoa siri ya Yule Mtawa,
Mfalme akaamuru kukamatwa kwa Mtawa na
kupelekwa kwako na akamtaka aache dini yake. Mtawa Yule akakataa kuacha dini
yake.
Mfalme akaamrisha kuwekwa msumeno na kukatwa pande zke mbili za kiwiliwili na akakatwa kichwa chake, mpaka zikaanguka pande zake mbili. Mfalme akamgeukia Yule Kipofu na kumuamrisha kurejea katika dini yake nae akakataa. Akauweka msumeno katika mgawanyiko wa kichwa chake, Mpaka zikaanguka pande zake mbili chini na akamwambia Yule kijana rejea uiache dini yako-akakataa akampeleka pamoja na kundi la watu kwenye jabali Fulani na akasema: Mtakapofikia kileleni kwake iwapo atarejea na kuiacha dini yake mwacheni na kama hatorejea kuiacha dini yake hapo mporomosheni, wakaenda nae walipofika naye jabalini akasema : ‘Ee Mola wangu waki nitosheleze na wao kwa lile ulitakalo, likatetemeka jabali wakaporomoka wote.
Mfalme akaamrisha kuwekwa msumeno na kukatwa pande zke mbili za kiwiliwili na akakatwa kichwa chake, mpaka zikaanguka pande zake mbili. Mfalme akamgeukia Yule Kipofu na kumuamrisha kurejea katika dini yake nae akakataa. Akauweka msumeno katika mgawanyiko wa kichwa chake, Mpaka zikaanguka pande zake mbili chini na akamwambia Yule kijana rejea uiache dini yako-akakataa akampeleka pamoja na kundi la watu kwenye jabali Fulani na akasema: Mtakapofikia kileleni kwake iwapo atarejea na kuiacha dini yake mwacheni na kama hatorejea kuiacha dini yake hapo mporomosheni, wakaenda nae walipofika naye jabalini akasema : ‘Ee Mola wangu waki nitosheleze na wao kwa lile ulitakalo, likatetemeka jabali wakaporomoka wote.
Akaja Yule kijana
akitafutatafuta mpaka akaingia kwa
mfalme akasema wamefanya nini wenzio?
Akasema amenitosha mimi Mwenyezi
Mungu Mtukufu. Mfalme akaamrisha apelekwe pamoja na watu katika jahazi ,
akasema mtakapingia baharini na huyo kijana iwapo atarejea kuiacha dini yake
mwacheni na kama hakurejea mzamisheni baharini. Wakaingia nae baharini akasema
Yule kijana,” Ee Mola wangu wa haki nitosheleze
na hawa kwa lile unalolitaka” wakazama majini wote.
Akaja kijana mpaka akaingia kwa
mfalme akauliza wamefanya nini wenzio akasema amenitosha nao Mwenyezi Mungu
mtukufu, Kisha Yule Kijana Akamwambia mfalme “ kwa hakika wewe hutaweza kuniua
mpaka ufanye lile nitakalokuamrisha” iwapo wewe utafanya lile nitakalokuamrisha hapo utaweza kuniua na kama
hukufanya basi wewe hutaweza kuniua, Mfalme akasema ni jambo gani hilo?Yule
kijana akajibu, Kusanya watu katika uwanja mmoja kasha unifunge katika shina la
mti na uchuke mshale wangun katika mkoba wake kasha sema, “Kwa jina la Mwenyezi
Mungu , Bwana wa Kijana Huyu” hakika wewe utakapofanya hivyo utaniua. Mfalme
akafanya kama alivyoambiwa akaweka
mshale katikatiya upinde kasha
akamfyatulia na akasema kwa jina la Mwenyezi Mungu Bwana wa Kijana huyu
kikatuka chombo cha mshale sehemu iliyo kati ya shavu na sikio akaweka kijana
mkono wake juu ya mahali pa mshale na akafa.
Watu wote wakasema: Tumemwamini
Bwana wa kijana, akaambiwa mfalme jee umelionalile ulilokuwa unalitahadhari?
Kwa hakika tunaapa kwa Mwenyezi Mungu limekwisha kukusukia kwa haika watu wote
wameamini, akaamrisha katika maingilio ya njia zote yakachimbwa mahandaki na
ukawashwa katika mahandaki hayo moto na akasema atakayerejea kuiacha dini yake
hiyo mwacheni, na kama hakurejea mtumbukizeni ndani ya moto wakawa wanaongezeka kwa idadi na wanashindana
kuingia motoni akaja mwanamke na motto wake hali ya kuwa anamnyonyesha kana kwamba alisita kuingia motoni, akasema
Yule motto:” “ Vumilia Ee Mama yangu kwa hakika wewe uko juu ya haki”