MIAKA MINNE (4) YA HUDUMA KWA JAMII

Assalamu Alaykum 

Awali ya yote hatuna budi tumshukuru Mungu ambaye kwa rahma yake ndiye aliyetupa muda mwingine huu wa kuishi katika hali mbalimbali za kiafya na kiuchumi.

Ndugu Msomaji Mtandao wako wa tibasahihi unafikisha miaka minne (4) ya huduma tangu kuanzaishwa kwake mnamo mwaka 2012 mwezi Juni ukiwa na lengo la kuielimisha jamii kuachana na vitendo vyote vya kishirikina katika hali zote za Maisha ya mwanadamu, iwe ni katika matibabu, ajira, biashara,Mahusiano,Madaraka N.k 

Na badala yake kuilekeza jamii katika kumuomba na kumtegemea Mungu Muumbaji na ndiye mlinzi anayetoa rizki kwa viumbe wake wote,

Katika kuadhimisha miaka 4 ya huduma hii nitawaletea baadhi ya simulizi kutokana na niliyoyashuhudia katika utoaji wa huduma hii.

kwa wanaohitaji huduma hii wawasiliane nami kwa simu namba 0715604488