Ndugu Msomaji
Tukiwa katika mwezi wa mwisho kuelekea katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kutokana na changamoto zinazowakabili baadhi ya waislam za kutokuwa na uhakika wa kupata futari wala daku (hali ambayo pia huwakuta hata siku zisizokuwa za mwezi wa Ramadhani kukosa mlo).
Tibasahihi blog imeona ni jambo la kheri kuendelea na utaratibu tuliouanzisha Ramadhan ya mwaka jana ambayo kwa kiasi fulani iliwezesha baadhi ya wahitaji kupata baadhi ya mahitaji.
Hivyo kwa kushirikiana nawe Msomaji wetu tujitahidi kutoa kila tulichonacho ili kuwasidia wahitaji hawa, tunaanza kupokea michango ili ikifika siku chache kabla ya Ramadhan kuanza au ndani ya Ramadhani, tuanze kugawa kwa walengwa hivyo basi tuma mchango wako sasa na kwa hakika kuna malipo makubwa mbele ya Allah pia izingatiwe kuwa Mtume swalla llaahu alayhi wasallam ameeleza malipo ya mwenye kumfuturisha aliyefunga ni sawa na malipo ya mfungaji mwenyewe.
Unaweza kutoa kwa ajili yako au kwa ajili ya anayekuhusu kama baba mama aliyetangulia mbele za haki na wengineo ambao wana udhuru wa kutofunga lakini wakiwajibikiwa na kufuturisha kama vile wazee sana au wagonjwa n.k
Unaweza kutuma mchango wako kwa kutumia namba 0715604488 Tigopesa au 0774339222 Easypesa.
Tunawashukuru ndugu zetu ambao wameshaitikia wito hakika Allah atawalipa ziada ya kile walichotoa.
Unaweza kutuma mchango wako kwa kutumia namba 0715604488 Tigopesa au 0774339222 Easypesa.
Tunawashukuru ndugu zetu ambao wameshaitikia wito hakika Allah atawalipa ziada ya kile walichotoa.