SHUKRAN ZA DHATI KWENU WASOMAJI WETU


 Msomaji Mpendwa
Assalaamu alaykum.

Awali ya yote tumshukuru  Allah kwa kutuwezesha kuwa miongoni mwa walio hai katika muda huu tena ndani ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani mwezi ambao wengi wetu walitamani nao kuupata ili waweze kujituma zaidi katika ibada ili waweze kupata  fadhila kubwa iliyopo ndani ya mwezi huu.

Ndugu Msomaji Blog yako ya TIBASAHIHI inakushukuru sana kwa ushirikiano wako mkubwa ulioutoa mara tu baada ya kupata wito huu wa kutoa ulichonacho ili kusaidia waislam wenzako kuweza kupata futari na daku, Alhamdulillah tumeweza kusaidia baadhi na kuna baadhi bado hatujaweza kuwapatia lakini kwa hiki  ulichokitoa hakika Allah atakubarik kwa rahma zake.

Pia tunatoa wito kwa wengine ambao hawakuwa wamefanikiwa kutoa mchango wao mwanzo wanaweza kutoa sasa na sio lazima ije kwetu bali unaweza kuangalia walio jirani nawe wenye kuhitaji na ukawasaidia hakika utakuwa umefanya jambo kubwa sana na In shaa Allah tarajia malipo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Mwisho wale wanaotaka kuendelea kusaidia kwa kutuma michango yao kwetu wanaweza kutumia namba ifuatayo:- Tigopesa 0715604488