BLOG YA TIBA SAHIHI:
TUNAIUNGA MKONO NA KUIOMBEA SERIKALI YETU

Assalaamu alaykum
Ndugu Msomaji
Kila Mtanzania anashuhudia juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali hii ya Awamu ya 5 inayoongozwa na Mh. Magufuli katika kuwaletea Maendeleo Watanzania.

Mpaka sasa tumeshaanza kuona muelekeo wa Tanzania katika siku zijazo watumishi wanasimamiwa na wanatekeleza majukumu yao na huku wakihofu kuharibu wakijua kuwa watawajibishwa, kuwepo kwa mfumo wa uwajibishaji (Utumbuaji Majibu) kunafanya umakini uongezeke katika kazi za kila siku.

Blogu ya TIBA SAHIHI ikiwa sehemu ya Mitandao ya kijamii yenye jukumu la kukemea tabia mbalimbali zisizofaa katika jamii, ikiwemo Kupinga Na kukemea tabia za Ushirikina ambao mara nyingi umekuwa ukisababisha Ukatili na mauaji kwa Ndugu zetu wasio na hatia ALBINO na Vikongwe na hivyo kurudisha nyumba maendeleo ya Taifa.

BLOGU YA TIBA SAHIHI inapenda kuchukua fursa hii kuipongeza na kuiunga Mkono serikali hii lakini pia tunaiombea kwa Mwenyezi Mungu aisimimie katika kututumikia Watanzania kwa uadilifu, kwani uadilifu husababisha kupatikana haki kwa kila Mmoja na haki hudumisha  Amani na amani huleta Utulivu na kisha ndio kunapatikana maendeleo katika jamii.

Hapo kila mmoja atajituma katika kujenga taifa (Kufanya kazi) kwa atakuwa na hakika ya kupata stahiki zake kwa wakati na kusaidia jamii yake.

"Ewe Mwenyezi Mungu Tunakuomba Uidumishe Amani iliyopo Nchi MWETU na UMSIMAMIE NA UMUONGOZE Rais  wetu Mh. Magufuli na Serikali yake WATUTUMIKIE KWA UADILIFU na UWALINDE dhidi ya Maadui wote".