Soma na Uzingatie Kisa hiki cha
MCHAWI,MTAWA NA KIJANA

Assalaamu Alaykum
Ndugu Msomaji
Kama ilivyo ada awali ya yote tuchukue fursa hii kumshukuru Allah mola mlezi wa viumbe wote yeye ndie aliyeumba mbingu na Ardhi na vilivyomo, hafanani na yeyote wala chochote hakika yeye Allah anasikia kila kitu na anaona kila kitu.

Kisa hiki anakisimulia mtume Muhammad Swalla llaahu alayhi wasallam kuwa “Alikuwepo katika watu waliokuwa kabla yenu Mfalme ambae alikuwa na mchawi.
Mchawi Yule alipokuwa mtu mzima sana kwa uzee wake alimwambia mfalme, “Hakika mimi limekuwa kubwa rika langu na nimehudhuria ajali yangu, nitafutie kijana nimfundishe uchawi. Mfalme akampelekea kijana  akawa anamfundihs uchawi na likuwa baina ya mchawi na mfalme mtawa wa kinaswara. Kijana Yule akaenda kwa Yule mtawa na akasikiliza mafundisho yake  ukamvutia ufasaha wake na maneno yake,  na  akawa  anapomwendea mchawi anampiga na kumwambia ni jambo gani lililokuchelewesha? Na akiwa anakwenda kwa watu wake humpiga na kumwambia ni jambo gani liliokuchelewesha? Yule kijana akaeleza  hali yake { ya kupigwa na Yule mchawi} kwa Yule mtawa, akamwambia  hakika mchawi akikupiga  sema wamenichelewesha watu wangu, na wakitaka watu wako kukupiga sema amenichelewesha mchawi.

Siku moja katika ada yake ghafla akiwa anakwenda kwa Yule matawa alitokea  mnyama mkubwa sana  amewazuia watu hawawezi kupita. Kwa kutokea jambo lile akasema leo nitaelewa jambo la mtawa je, linapendeza sana kwa mwenyezimungu au jambo la mchawi ndio lenye kupendeza? Amesema,  Mara kijana Yule akachukua jiwe akasema, ‘Ee Mola wangu wa haki likiwa jambo la mtawa linapendeza sana kwako na linaridhiwa sana kuliko jambo la mchawa basi muue mnyama huyo ili watu waweze kupita’ akamtupia jiwe mnyama Yule  na akamuua na watu wakapita.
Kijana akamueleza mtawa habari ile akasema:  ‘Ewe kijana change wewe ni mbora kuliko mimi na utapata majaribio, utakapopatwa na majaribio usiwafahamishe watu kuhusu mimi, ikawa kazi ya kijana Yule kuwaponesha  vipofu, na wenye mbalanga na baki ya magonjwa.

Mfalme alikuwa ana rafiki katika baraza lake akapofuka akasikia kuhusu habari ya za kijana Yule akamwendea na zawadi nyingi sana akamwambia  niponyeshe na utapata wewe vitu vyote nilivyo navyo. Yule kijana akasema Sikuwa mimi ninamponya mtu yeyote, hakika hapana jambo lolote nifanyalo ispokuwa Mwenyezi Mungu, mwenye kushinda , mwenye utukufu , ukimwamini nitamwomba na atakuponyyesha, Yule bwana akaamini – na Yule kijana akamuombea Mwenyezi Mungu na akapona.
Kisha akamwendea Mfalme akakaa kwake palepale alipokuwa anakaa, Mfalme akamuuliza “Eee Fulani ni nani aliyekurudishia  kuona kwako? Akasema: “Ni Bwana wangu, akasema: mimi? Akasema: Hapana  Bwana wangu na Bwana wako ni Mwenyezi Mungu.

Mfalme Akasema ,jee wewe una Bwana asiyekuwa mimi? Akasema: Ndiyo Bwana wangu na Bwana wako ni Mwenyezi Mungu. Mfalme akawa anamtesa hadi akajulishwa kuhusu kijana Yule, Mfalme akapeleka  ujumbe kwa Yule kijana akasema”  “ Ewe kijana change, umefikia katika uchawi wako kiasi cha kuwa unawaponyesha vipofu, na wenye mbalanga? Na magonjwa mengine haya? Yule kijana akasema mimi simponyeshi mtu yeyote  hakika  hapana jambo lolote bali anayeponyesha ni Mwenyezi Mungu , Mwenye Kushinda, Mwenye kutukuka, Mfalme akasema: Ni mimi? Kijana akajibu ‘hapana’ Mfalme akamuuliza  ‘Hivi wewe una Bwana mwingine asiyekuwa mimi? Kijana akasema:  Bwana wako na Bwana wangu ni Mwenyezi Mungu. Mfalme akamuadhibu kijana Yule kwa adhabu mbali mbali kiasi cha Yule kijana kutoa siri ya Yule Mtawa, Mfalme akaamuru kukamatwa kwa Mtawa  na kupelekwa kwako na akamtaka aache dini yake. Mtawa Yule akakataa kuacha dini yake.

Mfalme akaamrisha kuwekwa msumeno  na kukatwa pande zke mbili za kiwiliwili na akakatwa  kichwa chake, mpaka zikaanguka pande zake mbili. Mfalme akamgeukia Yule Kipofu na kumuamrisha kurejea katika dini yake nae akakataa. Akauweka msumeno katika mgawanyiko wa kichwa chake, Mpaka zikaanguka pande zake mbili chini  na akamwambia Yule kijana rejea uiache dini yako-akakataa akampeleka pamoja na kundi la watu kwenye jabali Fulani  na akasema: Mtakapofikia kileleni kwake iwapo atarejea na kuiacha dini yake mwacheni na kama hatorejea kuiacha dini yake hapo mporomosheni, wakaenda nae walipofika naye jabalini akasema : ‘Ee Mola wangu waki nitosheleze  na wao kwa lile ulitakalo, likatetemeka jabali wakaporomoka wote.

Akaja Yule kijana akitafutatafuta  mpaka akaingia kwa mfalme akasema wamefanya nini wenzio?  Akasema amenitosha mimi Mwenyezi  Mungu Mtukufu. Mfalme akaamrisha apelekwe pamoja na watu katika jahazi , akasema mtakapingia baharini na huyo kijana iwapo atarejea kuiacha dini yake mwacheni na kama hakurejea mzamisheni baharini. Wakaingia nae baharini akasema Yule kijana,” Ee Mola wangu wa haki nitosheleze  na hawa kwa lile unalolitaka” wakazama majini wote. 

Akaja kijana mpaka akaingia kwa mfalme akauliza wamefanya nini wenzio akasema amenitosha nao Mwenyezi Mungu mtukufu, Kisha Yule Kijana Akamwambia mfalme “ kwa hakika wewe hutaweza kuniua mpaka ufanye lile nitakalokuamrisha” iwapo wewe utafanya lile  nitakalokuamrisha hapo utaweza kuniua na kama hukufanya basi wewe hutaweza kuniua, Mfalme akasema ni jambo gani hilo?Yule kijana akajibu, Kusanya watu katika uwanja mmoja kasha unifunge katika shina la mti na uchuke mshale wangun katika mkoba wake kasha sema, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu , Bwana wa Kijana Huyu” hakika wewe utakapofanya hivyo utaniua. Mfalme akafanya kama alivyoambiwa akaweka  mshale katikatiya upinde  kasha akamfyatulia na akasema kwa jina la Mwenyezi Mungu Bwana wa Kijana huyu kikatuka chombo cha mshale sehemu iliyo kati ya shavu na sikio akaweka kijana mkono wake juu ya mahali pa mshale na akafa.

Watu wote wakasema: Tumemwamini Bwana wa kijana, akaambiwa mfalme jee umelionalile ulilokuwa unalitahadhari? Kwa hakika tunaapa kwa Mwenyezi Mungu limekwisha kukusukia kwa haika watu wote wameamini, akaamrisha katika maingilio ya njia zote yakachimbwa mahandaki na ukawashwa katika mahandaki hayo moto na akasema atakayerejea kuiacha dini yake hiyo mwacheni, na kama hakurejea mtumbukizeni ndani ya moto  wakawa wanaongezeka kwa idadi na wanashindana kuingia motoni akaja mwanamke na motto wake hali ya kuwa anamnyonyesha  kana kwamba alisita kuingia motoni, akasema Yule motto:” “ Vumilia Ee Mama yangu kwa hakika wewe uko juu ya haki”