HAKIKA HUU NDIO MSIMAMO WANGU,SISHUGHULIKI NA USHIRIKINA.

Msomaji Wangu Mpendwa,
Assalaamu alaykum
Awali ya yote napenda kumshukuru Allaah mola mlezi wa viumbe wote ambaye hana Mke, hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hakuna kilichompelekea kuwa na mke wala mtoto na wala hajapungukiwa na chochote,utukufu ni wake na sifa njema za ukamilifu ni zake,hana mshirika katika kuabudiwa wala hana mshirika katika ufalme wake hafanani na yeyote wala chochote na yeye anasikia kila kitu na anaona kila kitu na anajua kila kitu,kwa rehma na fadhila zake
ametujaalia kuwa ni katika wanaoishi muda huu tunaosoma blog hii ingawa sio ndio uhakika wa kuweza kumaliza kusoma hata post moja tukiwa hai Alhamdulillaah.Ziada ya Rehma na amani zimfikie kiongozi na mtume wa mwisho katika ulimwengu huu Mtume Muhammad S.A.W na Aali zake,Maswahaba zake na wote wataowafuata mpaka siku ya malipo.

Msomaji Wangu Mpendwa.
Nikushukuru na wewe kwa kuwa mmoja wapo wa wasomaji wa blog hii na kuifanya kazi ngumu ya kulingania waja wa mungu kuwa na wepesi kiasi kwani kama sio rehma za Allaah kuwezesha wanaadamu kutengeneza mitandao kama hii nisingeweza kukufikia wewe hapo ulipo katika muda huu na kukueleza haya yaliyomo humu ambayo ninaamini kuwa wapo wengi ambao yamewanufaisha na kuwarudisha kwa idhini ya Allaah katika kundi la waja wa Allaah na kuwafanya wajitambue kiasi cha kuepuka ushirikina.kwam njia hii nimeshawafikia wasomaji kutoka nchi nyingi  miongoni mwazo ikiwemo TANZANIA ni KENYA,UGANDA,BURUNDI,OMAN QATAR,SWEDEN,GERMAN,TURKEY,SPAIN,INDONESIA,
HOLLAND,UK,U.S.A,CANADA SAUDI ARABIA,


UBAYA AU MADHARA YA USHIRIKINA KATI YA MTU NA MUUMBA WAKE

Msomaji Wangu Mpendwa,
Kilichonipelekea kuanzisha blog hii ni kutamani kuwafikia walimwengu kwa urahisi na kuwabainishia ubaya wa ushirikina kati ya MJA na MUUMBA WAKE kama ALLAAH anavyosema kwenye  kitabu chake kitukufu kuwa mwenye kumshirikisha Allaah, basi Allaah amemuharamishia mtu huyo pepo na mafikio yake ni motoni na mwenye kumshirikisha Allaah Amali zake njema zote zinaporomoka yani zinaharibika  na atakuwa katika waliopata hasara kubwa.nikisema kumshirikisha Allaah na kusudia kuomba ambacho hakuna awezaye kukusaidia ispokuwa yeye kama vile kuomba mvua inyeshe au kuomba mvua iache kunyesha kutokana na madhara au maafa makubwa yaliyosababishwa na kunyesha kwake au kuomba ulinzi dhidi ya wachawi au mashetani sasa utakuta mtu anasumbuliwa na mashetani badala ya kumuomba ponyo na kinga Allaah yeye anaenda kwa waganga washirikina wanamchanja na kumvalisha mahirizi mwilini, waganga washirikina utawatambua ukiona vitu vifuatavyo:-wanatumia mavazi ya rangi maalum kama vile rangi nyekundu,nyeupe au nyeusi iwe wanatumia zote kwa pamoja au mojawapo,pili wana tabia za kuulizia majina ya mama au kukuagiza upeleke kucha,nywele au kipande cha nguo n.k 

UBAYA AU MADHARA YA USHIRIKINA KATI YA MTU NA WANAJAMII ANAOISHI NAO.

Ama nikigeukia upande wa ushirikina na washirikina kati yao na jamii inayowazunguka kwanza kabisa utakosa ushirikiano na watu kwa sababu wakikutwa na maradhi ya ajabuajabu au kupotelewa na mali zao katika mazingira ya kutatanisha na wewe umeshaonekana kuwa unapenda mambo ya kishirikina watajua ni wewe na hapo ndio utakuta jamii nzima inayokuzunguka inakutenga ama kwa wewe unaefanya ushirikina kwa kwenda kwa waganga wapiga ramli watakuchonganisha hata na mkeo au mumeo au watoto wako pale utakapoambiwa kuwa mmoja wao ndio mmbaya wako,hivyo ushirikina unasababisha mifarakano na uadui katika jamii kitu ambacho uislam umekikataza.

CHANGAMOTO NINAZO KUTANA NAZO HUMU

Miongoni mwa changamoto ninazokutana nazo ni kueleweka vibaya na baadhi ya wasomaji wangu kwa kudhani kwamba mimi nishughulika na uchawi au kuwasaidia watu wafanikiwe katika njia za kichawi au kijini na changamoto hii zaidi nimekuwa nikiipata kwa wasomaji wangu wa hapa nyumbani Tanzania na zaidi wanatokea mikoa fulani hivyo nawakumbusha wasomaji wangu kuwa sishughuliki na njia za kumsaidia mtu kupata utajiri wa kijini wala sishughuki na kutoa pete za bahati wala sipigi ramli,wengine wanasema wako tayari kuwatoa kafara ndugu zao au watoto zao au wazazi ama wake na waume zao jamani muogopeni ALLAAH na jueni kuwa hamtaishi milele, kwani kuna wachawi wangapi wameshakufa? au wangapi waliowatoa kafara wapendwa wao wameshakufa? je wapiga ramli wangapi wameshakufa? je nyinyi mtabaki milelena wengine wananipigia na kuniuliza kama nipo Nigeria wakati wanaona namba ni za Tanzania! ndugu zangu nawasihi msitengeneze mazingira ya kutapeliwa sasa ningesema kama mimi ni Mnigeria ndio ingekuwaje?Mimi ni Mtanzania na ninapinga na kukemea ushirikina ili nipate radhi za ALLAAH nawe nakukaribisha ushirikiane nami kwa kunishauri au kuniuliza maswali nipigie kwa namba zangu zilizopo hapo juu,Sijibu sms kwa mtu ninaewasiliana nae kwa mara ya kwanza.    Mpendwa Msomaji wangu ili kupata haya na mengineyo  nifuatilie kupitia twitter kwa kuponyeza hapa https://twitter.com/HemediPalike

EWE MWENYEZIMUNGU SHUHUDIA KUWA NIMEWAFIKISHIA WAJA WAKO.