Ndugu Msomaji,
Katika Miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia kukithiri kwa vitendo vya kikatili dhidi ya Vikongwe na Walemavu wa Ngozi Albino.
Katika Miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia kukithiri kwa vitendo vya kikatili dhidi ya Vikongwe na Walemavu wa Ngozi Albino.
Tumekuwa tukishuhudia na kusikia kuuawa kwa Watanzania hawa dhaifu huku wengine wakiachwa wakiwa hawana baadhi ya sehemu za viungo vyao, imekuwa ikionekana kama ni kawaida kusikia sehemu fulani ameuawa kikongwe, au ameuawa Albino ama amekatwa kiungo/viungo.
Vitendo hivi hutekelezwa na watu waliokosa matunzo na malezi sahihi ya kiroho ya kujua thamani ya kila Binadamu,Lengo La kuumbwa kwake na kutojua ama kuamini juu ghadhabu za Mungu Muumbaji kwa yule anayedhulumu haki za wengine ikiwepo haki ya kuishi kwa vyovyote binaadamu anayejitambua na kuyatambua haya hawezi kudiriki kufanya mauji na ukatili huu kwa tamaa yoyote ile iwe ya kupata utajiri ama madaraka/vyeo.
KWANINI WATANZANIA HAWA WANAUAWA?
Kwa upande wa Vikongwe mara nyingi huhusishwa na vitendo vya kichawi watu wasiokuwa na huruma na watanzania wenzao wameshajiwekea alama ambazo huzitumia 'kuwatambua wachawi'wakimuona mtu ana macho mekundu basi kwao mtu huyo ni mchawi na hukumu yake ni kuuawa hii sio sahihi kwani wapo vijana wadogo tu ambao ni wachawi.
Ama hawa Walemavu wa Ngozi mara nyingi huuawa ama kukatwa viungo vyao, Makatili hawa ambao ni zaidi ya wanyama hutekeleza unyama wao huu kwa kisingizio tena baada ya kudanganywa na waganga washirikina kuwa viungo wa Albino vinaweza kuwatajirisha kitu ambacho ni uwongo ulio dhahiri, vitendo Hivi vinaathiri kwa kiwango kikubwa uchumi na nguvu kazi ya taifa, natoa wito kwa watanzania wenzangu wapenda amani kushikamana kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika na usalama wa nchi yetu Katika kupambana na hatimaye kutokomeza vitendo Hivi visivyo vya kibinadam, tutoe ushirikiano wa kutosha kwa mamlaka hizi ili ziweze kutekeleza wajibu wa kutulinda raia wa nchi hii ipasavyo, tusifumbie macho vitendo hivi viovu na vinginevyo vyenye viashiria vya kuvunja amani yetu.
Kwani haya ni miongoni mwa madhara ya kukumbatia imani na vitendo vya kishirikina hakika hatupaswi kuvifumbia macho vitendo hivi na sasa ni wakati wa kuamini kuwa kila ambalo limekemewa na Allah Muumba wa Mbingun na Ardhi lina madhara makubwa na tumekatazwa kwa manufaa yetu lau watu wangetii amri ya mungu basi tusingekuwa na majanga haya tuliyonayo.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Tubariki Watanzania.