KINGA MADHUBUTI DHIDI YA SHARI ZOTE-1
Msomaji wangu Mpendwa
Assalaam alaykum,
Kabla ya yote napenda nichukue fursa hii adimu ya pumzi nimshukuru Allaah muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake na baina yake kwa fadhila zake ametujaalia kuwa hai katika muda huu tukikutana tena katika mtandao wetu huu tukiendelea kuelimishana mambo mbalimbali yahusuyo KINGA & TIBA SAHIHI
isiyokuwa ya kishirikina na mafundisho ya dini ya kiislam, rahma na amani ya Allah imfikie Mtume Muhammad S.A.W na Aali zake na sahaba zake wote na wote watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya malipo.
Leo nimependelea kuwaletea somo hili la kinga madhubuti dhidi ya kila shari ikiwa ni majibu ya maombi ya wasomaji wangu mbalimbali ambao wamekuwa wakinitaka niwape kinga ili wasidhuriwe na chochote!
Kinga nitakayowaelekeza mimi ni ile iliyoelekezwa na Qur'aan na Sunnah ama kimoja wapo kati ya viwili hivyo na sio vinginevyo maana wasomaji wengine hudhani kuna kitu watapewa ili kiwakinge kama wanavyofanyiwa na washirikina,
Ndugu yangu Uislam ni Mfumo wa Maisha uliokamilika hivyo hata kinga imeelekezwa humo na haina ugumu wowote wewe unachotakiwa ni kusoma tu haya nitakayokuelekeza Inshaa Allah utakuwa umeshajipatia kinga madhubuti.
Hii ni kinyume na kinga za washirikina za kuvaa hirizi ama kuchanjwa sehemu mbalimbali za mwili vitendo hivyo ni haramu Allaah havipendi na ninawaasa ndugu zangu tuviepuke na badala yake tuelekee kule ambapo Muumba wetu ametuelekeza.
1) Kinga ya kwanza:
Ni kujikinga kwa Allah kwa kusema
أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
"A'uudhu billaahi minas shaytwaanir rajiim".
kila unapokuwa na hasira au *unapomsikia mbwa anabweka ama punda,
*kwani Mtume Swalla llaahu 'alayhi wasallam ameeleza kuwa ukiwasikia viumbe hao wanabweka basi jikinge kwa Allaah dhidi ya shetani kwani watakuwa wamemuona Shetani.
''Na Shet'ani akikuchochea kwa uchochezi wewe jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua''. Fussilat :36
2)Kinga ya Pili
Kusoma Mu'awwidhaati (Kinga)
Kwani Mtume Swalla llaahu 'alayhi wasallam ameelekeza kuzisoma pamoja na suuratul Ikhlaas mara tatu asubuhi na jioni huku ukijipulizia katika viganja n kujipangusa sehemu inapofika mikono yako na kwamba anayezisoma atakingwa na kila kitu. nazo ni hizi zifuatazo:-