MLANGO WA TWAHARA - 1
Fasili Ya Twahara Na Umuhimu Wake
Twahara katika lugha ya kawaida: Ni usafi na kumalizana na uchafu
au takataka za kihisia kama vile najisi kutokana na mkojo au kinginecho, na
uchafu wa kidhahania kama kasoro (mapungufu) na maasi. Na kutwaharisha ni
kusafisha, nako ni kuthibitisha usafi katika mahala.
Na Twahara kisheria (kitaaluma):
Ni kuondosha kile chenye
kuzuia swala kutokana na hadathi au najisi kwa kutumia maji (au kinginecho) au
kuondosha hukumu yake kwa mchanga.
Ama hukumu ya Twahara, bila shaka Twahara ya kilichonajisika na
kukiondosha ni jambo la wajibu ikiwa mtu atakumbuka na ataweza. Allaah
(Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:
((ﻭَﺛِﻴَﺎﺑَﻚَ ﻓَﻄَﻬِّﺮْ))
«Na nguo zako
zitwaharishe» (Al-Mudath-thir: 4)
Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((ﺃَﻥ ﻃَﻬِّﺮَﺍ ﺑَﻴْﺘِﻲَ ﻟِﻠﻄَّﺎﺋِﻔِﻴﻦَ
ﻭَﺍﻟْﻌَﺎﻛِﻔِﻴﻦَ ﻭَﺍﻟﺮُّﻛَّﻊِ ﺍﻟﺴُّﺠُﻮﺩِ))
«Ya kwamba itakaseni Nyumba Yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa
kutufu na wanaojitenga humo kwa ibada, na wanaoinama na kusujudu»( Al-Baqarah:
125)
Ama kujitwaharisha na hadathi, hilo ni lazima ili kuruhusika
kuswali, kwa neno lake Mtume(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
(( ﻻ ﺗﻘﺒﻞ ﺻﻼﺓ ﺑﻐﻴﺮ ﻃﻬﻮﺭ))
((Swalah
haikubaliwi bila ya wudhuu)) ( Swahiyh Muslim)
Ama umuhimu wake, bila shaka Twahara:
1- Ni sharti ya kusihi kwa swala ya mja.
Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((ﻻ ﺗﻘﺒﻞ ﺻﻼﺓ ﻣﻦ ﺃﺣﺪﺙ ﺣﺘﻰ ﻳﺘﻮﺿﺄ))
((Haikubaliwi swala ya mtu mwenye hadathi mpaka atawadhe)) (Al-Bukhaariy na Muslim)
Kwani kuswali na Twahara ni kumtukuza Allaah. Na hadathi na janaba
– ingawa si najisi zenye kuonekana – lakini hata hivyo ni najisi za kidhahania
zenye kuwajibisha kuonekana kichafu kile kilichoingiwa nazo. Kwa hiyo kuwepo
kwake, huteteresha ukamilifu wa kumtukuza Allaah, na huenda kinyume na msingi
wa usafi.
2- Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewasifu wenye kujitwaharisha.
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amesema
:
ُ ((ﺇِﻥَّ ﺍﻟﻠّﻪَ
ﻳُﺤِﺐُّ ﺍﻟﺘَّﻮَّﺍﺑِﻴﻦَ ﻭَﻳُﺤِﺐُّ ﺍﻟْﻤُﺘَﻄَﻬِّﺮِﻳﻦَ
«Hakika Allaah Anawapenda wenye kutubia na Anawapenda wenye
kujitwaharisha»
( Al-Baqarah:
222)
Itaendelea.......