MLANGO WA TWAHARA -2
Ama hukumu ya Twahara, bila shaka Twahara ya kilichonajisika na
kukiondosha ni jambo la wajibu ikiwa mtu atakumbuka na ataweza. Allaah
(Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:
((ﻭَﺛِﻴَﺎﺑَﻚَ ﻓَﻄَﻬِّﺮْ))
«Na nguo zako
zitwaharishe» (Al-Mudath-thir: 4)
Ama kujitwaharisha na hadathi, hilo ni lazima ili kuruhusika
kuswali, kwa neno lake Mtume(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
(( ﻻ ﺗﻘﺒﻞ ﺻﻼﺓ ﺑﻐﻴﺮ ﻃﻬﻮﺭ))
((Swalah
haikubaliwi bila ya wudhuu)) ( Swahiyh Muslim)
Ama umuhimu wake, bila shaka Twahara:
1- Ni sharti ya kusihi kwa swala ya mja.
Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((ﻻ ﺗﻘﺒﻞ ﺻﻼﺓ ﻣﻦ ﺃﺣﺪﺙ ﺣﺘﻰ ﻳﺘﻮﺿﺄ))
((Haikubaliwi swala ya mtu mwenye hadathi mpaka atawadhe)) (Al-Bukhaariy na Muslim)
Kwani kuswali na Twahara ni kumtukuza Allaah. Na hadathi na janaba
– ingawa si najisi zenye kuonekana – lakini hata hivyo ni najisi za kidhahania
zenye kuwajibisha kuonekana kichafu kile kilichoingiwa nazo. Kwa hiyo kuwepo
kwake, huteteresha ukamilifu wa kumtukuza Allaah, na huenda kinyume na msingi
wa usafi.
2- Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewasifu wenye kujitwaharisha.
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amesema
:
ُ ((ﺇِﻥَّ ﺍﻟﻠّﻪَ
ﻳُﺤِﺐُّ ﺍﻟﺘَّﻮَّﺍﺑِﻴﻦَ ﻭَﻳُﺤِﺐُّ ﺍﻟْﻤُﺘَﻄَﻬِّﺮِﻳﻦَ
«Hakika Allaah Anawapenda wenye kutubia na Anawapenda wenye
kujitwaharisha»
( Al-Baqarah:
222)
Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewasifu watu wa Msikiti wa Qubaa
kwa neno Lake:
((ﻓِﻴﻪِ ﺭِﺟَﺎﻝٌ ﻳُﺤِﺒُّﻮﻥَ ﺃَﻥ
ﻳَﺘَﻄَﻬَّﺮُﻭﺍْ ﻭَﺍﻟﻠّﻪُ ﻳُﺤِﺐُّ ﺍﻟْﻤُﻄَّﻬِّﺮِﻳﻦَ))
«Ndani yake kuna watu wanaopenda kujitwaharisha, na Allaah
Anawapenda wenye kujitwaharisha»
( At-Tawbah:
108)
3- Kwamba kutojali
kujitakasa na najisi, ni moja kati ya sababu za kuadhibiwa kaburini.
Imepokelewa na Ibn 'Abbaas akisema: Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) alipita kwenye makaburi mawili akasema:
((ﺇﻧﻬﻤﺎ ﻳﻌﺬﺑﺎﻥ ﻭﻣﺎ ﻳﻌﺬﺑﺎﻥ ﻓﻲ ﻛﺒﻴﺮ ﺃﻣﺎ ﻫﺬﺍ
ﻓﻜﺎﻥ ﻻ ﻳﺴﺘﻨﺰﻩ ﻣﻦ ﺑﻮﻟﻪ))
((Hakika wao (maiti) wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa.
Ama huyu, alikuwa hajitakasi na mkojo wake…))
( Abu Daawuud,
An-Nasaaiy, Ibn Maajah, ikiwa na isnaad Swahiyh)
Itaendelea...