MLANGO WA TWAHARA-04
Je, Pombe Ni
Katika Vitu Najisi?
Wanazuoni wamehitilafiana juu ya hukumu ya pombe katika kauli
mbili:
Kauli ya kwanza:
Ni najisi.
Haya ni madhehebu ya karibu Maulamaa wote. Kati yao ni Maimamu
wanne, na Shaykh wa Uislamu amelichagua. Na hoja yao ni neno Lake Subhaana:
«Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi, kamari, kuabudu masanamu na
kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya shetani. Basi jiepusheni navyo ili mpate
kufanikiwa».
Wamesema: Uchafu "Rijsu" ni najisi, wakahukumu unajisi wa
pombe yenyewe kama ni najisi ya kihisia.
Kauli ya pili:
Ni Twahara.
Kauli hii wameisema akina Rubay'i, Al-Layth, Al-Muzany na watangu
wema wengineo. Na imetiliwa nguvu na Ash-Shawkaany, As-Swan'aany, Ahmad Shaakir
na Al-Albaaniy (Allah Awarehemu) . Na hii ndio yenye nguvu kwa dalili
zifuatazo:
1- Ni kwamba katika aya hakuna dalili juu ya unajisi wa pombe. Na
hii ni kwa njia zifuatazo:
(a)
Ni kwamba neno uchafu
"rijsu", ni katika maneno ya visawe, kwani linabeba maana nyingi.
Kati ya maana hizo ni kitu kichafu, kitu kilichoharamishwa, kitu kibaya,
adhabu, laana, ukafiri, shari, dhambi, najisi na kadhalika.
(b) Ni kwamba
"sisi hatujakuta" au kugundua kauli ya mwanasalafi yeyote aliyefasiri
"Ar-Rijsu" katika aya hii kwa maana ya najisi, bali Ibn 'Abbaas
amesema: "Ar-Rijsu" ni hasira". Na Ibn Zayd amesema:
"Ar-Rijsu ni shari".
(c) Kwamba neno
"rijsu", mbali na aya hii, limekuja katika Kitabu cha Allaah katika
pahala patatu, na hakuna pahala popote kati yake ambapo "rijsu" ina
maana ya najisi.
Katika neno
Lake Subhaana:
«Namna hivi
Allaah Anajaalia uchafu (adhabu) juu ya wasioamini»,
neno
"Ar-Rijsu", maana yake ni adhabu. Na katika neno Lake Subhaana kuhusu
wanafiki:
Hakika hao ni najisi, na makazi yao ni
Jahannam.
Makusudio ni
kuwa vitendo vyao ni vichafu, yaani ni vibaya.
Na katika neno
Lake Subhaana:
«Basi
jiepusheni na uchafu wa masanamu».
Masanamu
yameitwa uchafu kwa vile yenyewe ndio sababu ya makamio na adhabu, na wala
makusudio sio najisi ya kihisia. Kwani mawe yenyewe na masanamu si najisi
(d) Na
ilipotukia pombe katika aya kuwa imeambatana na masanamu na upigaji ramli,hilo
limekuwa ni kiashirio chenye kuengua maana ya uchafu kupelekea katika unajisi
usio wa kisheria. Na ndivyo hivyo hivyo katika kauli Yake Subhaana:
"Hakika
washirikina ni najisi"
zilipokuja
dalili sahihi zenye kuhukumia kutokuwa najisi miili ya washirikina.
(e) Kwamba
kuharamishwa pombe, hakuwajibishi unajisi wake. Ama najisi, ni lazima
iharamishwe, kwani ni haramu kuvaa hariri na dhahabu ingawa vyenyewe ni Twahara
ikiwa ni udharura wa kisheria na kwa makubaliano ya wote
(f) Kwamba neno
"Ar-Rijsu" katika aya limezungushiwa mpaka (muqayyad) kuwekwa ndani
ya (kati ya kazi ya shetani). Kwa hiyo ni uchafu wa kivitendo, kwa maana ya
kibaya au kilichoharamishwa au dhambi, na wala si uchafu wa kiini cha kitu wa
kuvifanya vitu hivi kuwa ni najisi
2- Na kati ya
vinavyotolewa ushahidi juu ya utwahara wa pombe ni aliyoyasema Anas katika kisa
cha kuharamishwa pombe. Anasema: "…Na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) akamwamrisha mwenye kunadi atangaze: Jueni kwamba pombe
imeharamishwa,…". Akasema: "Nikatoka nikaimwaga ikatiririka katika
barabara za Madina
3- Na katika
kisa cha mtu aliyekuwa na mapipa mawili ya pombe
(…Na Mtume
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hakika Allaah
Aliyeharamisha kuinywa, Ameharamisha kuiuza))
Na mtu yule akayafungulia
mapipa mawili mpaka vikamalizika vilivyomo ndani yake…). Na lau kama pombe
ingelikuwa ni najisi, basi Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
angeliamrisha kumwagia maji juu ya ardhi ili kuitwaharisha kama alivyoamrisha
kumwagia maji juu ya mkojo wa bedui, na angeliwaamuru kujikinga nayo pombe.
4- Kwamba asili
yake ni Twahara. Na wala hanukuu kuhusu utwahara huo ila kinukuu sahihi. Na
hakuna dalili yoyote juu ya unajisi wake na kwa hivyo, inabakia juu ya asili.
Haya utambue
basi hata kama sio najisi lakini ni haramu kuinywa.
"Je,
Matapishi Ya Mwanaadamu Ni Najisi?"
Tumetangulia
kusema mara nyingi kwamba asili ya vitu vyote ni twahara, na kwamba
havihamishwi toka kwenye asili yake ila kwa kihamisho sahihi cha kutolea hoja,
kisichopingana na kile chenye kutiliwa nguvu au kuwa sawa nacho. Na ikiwa
tutalipata hilo, basi ni vizuri. Na kama hatukulipata hilo, itatulazimu
tusimame msimamo wa kumpinga anayedai kuwa ni najisi. Kwani kudai huku kuna
maanisha kwamba Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewajibisha kwa waja
Wake kuviosha vitu hivyo vinavyodaiwa kuwa ni najisi, na kwamba kuwepo kwake
kunazuia kuswali navyo. Basi ni ipi dalili ya hilo?!
Na matapishi na
mfano wa vitu kama hivi, hakikuthibiti kwa njia sahihi (ya kuaminika) chenye
kuyahamisha toka kwenye utwahara wa asili.
Na imepokelewa
kuhusu matapiko kauli ya 'Ammaar akisema: "Hakika utaosha nguo yako
iliyoingiwa na mkojo, kinyesi, matapishi, damu na manii".
Lakini kauli
hii ni dhaifu haitolewi hoja. Na Allah Ndiye Mjuzi zaidi.
Na imethibiti
toka kwa Abu Ad-Dardaai akisema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam) alitapika, akafungua na akatawadha (Hadiyth sahihi: Imetolewa na
Abuu Daawuud (2381), na At-Tirmidhiy (87), Ahmad (6/443) na wengineo)
Katika maelezo
haya, hakuna kiashirio chochote juu ya unajisi wa matapishi, na wala hakuna
dalili juu ya ulazima wa kutawadha akitapika mtu, na wala hayaonyeshi kuwa
wudhuu unatenguka kwayo, bali lengo lake ni kusunisha mtu atawadhe anapotapika.
Kwani kwa kitendo tu cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam),
hakuonyeshi kuwa ni wajibu.
Pamoja na hayo,
si kila chenye kutengua wudhuu kinahesabiwa kuwa ni najisi. Na Ibnu Hazmi
amelielekea hili na akalichagua Shaykh wa Uislamu katika (Al-Fataawaa).
"Nini
Hukumu Ya Majimaji (utoko) Yanayotoka Kwenye Utupu Wa Mwanamke Na Kile
Kiitwacho Unyevunyevu Wa Utupu Wa Mwanamke?"
Maulamaa wana
mielekeo miwili kuhusu unyevunyevu wa utupu wa mwanamke: ( Al-Mughny (2/88), na
Al-Majmu'u (1/570))+
WA KWANZA
Ni najisi, kwa
vile mtoto haumbwi katika utupu kufananisha na madhii. Wametolea dalili kwa
maelezo ya Zayd bin Khaalid kwamba alimuuliza 'Uthmaan bin ‘Affaan (Allaah
Amridhie) akisema: "Nieleze, (nini hukumu) mtu anapomwingilia mkewe na
wala hakumwaga manii? Akasema 'Uthmaan: "Atatawadha kama anavyotawadha kwa
ajili ya Swalah, na ataiosha dhakari yake". 'Uthmaan akasema:
"Nimeyasikia toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam)….". (Isnad sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (292), na
Muslim (347), lakini imefutwa (mansuukh))
Na maelezo ya
Ubayy bin Ka'ab kwamba yeye alisema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mtu
akimwingilia mkewe na wala hakumwaga? Akasema:
(ﻳﻐﺴﻞ ﻣﺎ ﻣﺲ ﺍﻟﻤﺮﺃﺓ ﻣﻨﻪ ﺛﻢ ﻳﺘﻮﺿﺄ ﻭﻳﺼﻠﻲ)
((Ataiosha
sehemu aliyomgusa nayo mwanamke, kisha atatawadha, na ataswali)) (Isnad sahihi:
Imetolewa na Al-Bukhaariy (293), na Muslim (346), nayo imefutwa (mansuukh))
Wamesema: Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuamrisha kuiosha sehemu
iliyogusana na utupu wa mwanamke ni dalili juu ya unajisi wa unyevu wa utupu wa
mwanamke.
Mimi ninapinga
(Abuu Maalik) nikisema kwamba Hadiyth hizo mbili zimefutwa (Angalia kwenye
"Fathul Baary" (1/473))
na Hadiyth
nyingine zenye kuamrisha kuoga kama itakavyokuja katika sehemu yake
inshaAllaah.
Na pia kuna
uwezekano wa kuwa amri ya kuosha ni kutokana na madhii yanayomtoka mwanamume au
mwanamke.
Vile vile
wametolea ushahidi juu ya unajisi wa (majimaji hayo) kwa kuwa kwake yanatoka
katika moja ya njia mbili. Na kanuni inasema:
"Chenye
kutoka katika njia mbili, basi ni najisi isipokuwa manii".
WA PILI
Kwamba majimaji
ya utupu ni twahara (Angalia kwenye "Jaami'i Ahkaamu An-Nasaaiy"
(1/68) cha Shaykh wetu Mustwafa bin Al-'Adawy Allah Amhifadhi)
Mwelekeo huu
unatolewa dalili kwa yafuatayo:
1- Kwamba
'Aaishah - Allaah Amridhie,- alikuwa akiyakwangua manii kutoka katika nguo ya Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yakiwa yametokana na kukutana
kimwili, kwani Mtume kamwe hakuota
(Hivi ndivyo alivyosema katika
"Al-Mughny" (2/88). Na Shaykh wetu amesema: "Hili linahitajia
matini toka katika Qur-aan au Hadiyth, na wala hatukuikuta matini katika mfano
wa hili")
na ilhali yeye anakutana na umajimaji wa
utupu. Na kwa vile sisi, lau kama tungelihukumia unajisi wa utupu wa mwanamke,
basi tungelihukumu unajisi wa manii yake. Kwani manii hayo yanatokea kwenye
utupu wake, na kwa hivyo yananajisika kwa unyevunyevu wake.
2- Kwamba
majimaji haya ni jambo ambalo liko wazi, nayo huwatoka sana wanawake. Na hakuna
shaka kwamba jambo hili lilikuwepo kwa wanawake katika enzi za Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyo kwa wanawake wa zama zetu
hizi. Na wala haikupokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) aliwaamrisha kuoga (kuosha) au kutawadha kutokana na hali hiyo.
3- Kwamba kauli
ya Maulamaa isemayo "Kila chenye kutoka kwenye njia mbili ni najisi
isipokuwa manii", basi hii si kauli iliyopokelewa toka kwa Aliyehifadhiwa
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na wala kauli hii
haijafanyiwa ijmaa ya Ummah.Bali imepokelewa kwamba baadhi ya vinavyotoka toka
kwenye njia mbili havitengui wudhuu, kama vile damu ya istihaadha kama
itakavyokuja katika mahala pake inshaAllah.
Ninasema (Abuu
Maalik): Ninaloliona mimi ambalo lina nguvu, ni kwa ufafanuzi huu:
"Ikiwa
majimaji haya yanamtoka mwanamke wakati wa kuchezeana na mumewe, au wakati ana
hamu ya kujamiiana na mfano wa hili hasa, basi hayo ni madhii. Na mimi nimejua
kwamba madhii ni najisi ambayo ni lazima ioshwe, na ni yenye kutengua wudhuu.
Ama ikiwa
majimaji haya yanatoka kwenye utupu wa mwanamke takriban nyakati zote, na yanazidi
wakati wa ujauzito, au wakati anapofanya kazi kwa bidii, au anapotembea mwendo
mrefu, basi majimaji hayo ni twahara kiasili kwa kutokuwepo dalili juu ya
unajisi wake. Na Allah Ndiye Mjuzi zaidi
"Najisi
Zinazosamehewa"
Kuna kauli
mbalimbali za Maulamaa kuhusu aina na kiasi cha najisi ambayo inaweza kuingia
katika nguo au mahala au mwilini na inakuwa ni yenye kusamehewa.
("Al-Fiqhu
Al-Islaamy wa Adillatuhu" (169-177))
Isipokuwa
kidhibiti cha najisi zinazosamehewa ni (kuwepo) udharura, kuenea kwa wingi
pamoja na kuwa ni vigumu kujikinga nayo, na kuwepo tabu na uzito mkubwa katika
kuiondosha.
<<Namna Ya Kuzitwaharisha Aina
Mbalimbali Za Najisi Ambazo Matini Imekuja Kuzibainisha>>
1-
Kuitwaharisha nguo kutokana na damu ya hedhi
Inakuwa ni kwa
kuikwangua na kuigandua, kisha kuisugua kwa ncha za vidole iachiane na itoke,
kisha ataiosha kwa maji. Ni kutokana na maelezo ya Asmaa binti Abu Bakr,
amesema: "Mwanamke mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mmoja wetu nguo yake
ikiingiwa na damu ya hedhi, afanyaje"? Akasema Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam):
ﺗﺤﺘﻪ, ﺛﻢ ﺗﻘﺮﺻﻪ ﺑﺎﻟﻤﺎﺀ ﺛﻢ ﺗﻨﻀﺤﻪ, ﺛﻢ ﺗﺼﻠﻲ ﻓﻴﻪ)
((Ataipikicha,
kisha ataikwangua kwa ncha za vidole na maji, kisha atainyunyizia maji, na
kisha atasali nayo)) (Hadiyth sahihi: Ameitoa Al-Bukhaariy, na Muslim (291))
Na kwa maelezo
ya 'Aaishah, amesema: " Mmoja wetu alikuwa akipatwa na hedhi, kisha
huikwangua damu toka kwenye nguo yake wakati anapotwaharika, kisha huiosha, na
hunyunyizia maji sehemu iliyobaki, kisha huswali nayo". (Hadiyth sahihi:
Imetolewa na Al-Bukhaariy (308), na Ibnu Maajah (630))
Na kama
mwanamke atataka kutumia kijiti au kinginecho ili aondoshee damu, au aioshe
nguo kwa maji na sabuni na mfano wake katika madawa ya kusafishia, basi itakuwa
ni vizuri zaidi.
Hii ni kwa
maelezo ya Ummu Qays binti Muhaswan, amesema: "Nilimuuliza Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu damu ya hedhi iliyoingia kwenye
nguo. Akasema:
((ﺣﻜﻴﻪ ﺑﻀﻠﻊ، ﻭﺍﻏﺴﻠﻴﻪ ﺑﻤﺎﺀ ﻭﺳﺪﺭ))
((Ikwangue kwa
ujiti, na uioshe kwa maji na mkunazi)).
(Hadiyth hasan: Imetolewa na Abuu Daawuud
(363), na An-Nasaaiy (1/195), na Ibnu Maajah (268))
2-
Kuitwaharisha nguo kutokana na mkojo wa mtoto mchanga
Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((ﻳﻐﺴﻞ ﻣﻦ ﺑﻮﻝ ﺍﻟﺠﺎﺭﻳﺔ, ﻭﻳﺮﺵ ﻣﻦ ﺑﻮﻝ ﺍﻟﻐﻼﻡ))
((Huoshwa
ikiingia mkojo wa mtoto wa kike, na hurashiwa maji ikiingia mkojo wa mtoto wa
kiume)). (Hadiyth sahihi kwa nyingineyo: Imetolewa na Abuu Daawuud (376), na
An-Nasaaiy (1/158), na Ibnu Maajah (526))
3-
Kuitwaharisha nguo kutokana na madhii
Na kwa vile
madhii ni kitu kinachokithiri kutoka na kuenea kwa wengi, kuyatwaharisha
kumefanywa ni kwepesi na Mwekaji sheria. Kwa hiyo, inatosha kuinyunyizia nguo
maji sehemu iliyoingia madhii. Kwa Hadiyth ya Sahl bin Hunayf kwamba yeye
alikuwa akipata tabu na uzito kutokana na madhii. Akamwambia Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni vipi kwa yale yanayoingia katika
nguo yangu? Akasema:
((ﻳﻜﻔﻴﻚ ﺃﻥ ﺗﺄﺧﺬ ﻛﻔﺎ ﻣﻦ ﻣﺎﺀ ﻓﺘﻨﻀﺢ ﺑﻪ ﺛﻮﺑﻚ
ﺣﻴﺚ ﺗﺮﻯ ﺃﻧﻪ ﻗﺪ ﺃﺻﺎﺏ ﻣﻨﻪ))
((Inakutosha
kuchukua teko la maji, ukanyunyizia kwalo nguo yako pale unapoona yameingia)).
(Hadiyth hasan: Imetolewa na Abuu Daawuud
(383), na At-Tirmidhiy (143), na Ibnu Maajah (531))
4-
Kuitwaharisha sehemu ya nguo ya mwanamke inayoburuzika
Inaponajisika
sehemu ya nguo ya mwanamke inayoburuzika, basi hutwaharika kwa kugusana na
ardhi iliyo twahara. Mwanamke mmoja alimuuliza mke wa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) Ummu Salamah akimwambia: "Hakika mimi ni
mwanamke ninayerefusha ncha za nguo yangu na ninatembea sehemu chafu".
Ummu Salamah akamwambia: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
amesema:
((ﻳﻄﻬﺮﻩ ﻣﺎ ﺑﻌﺪﻩ))
((Huitwaharisha
(ardhi) iliyo baada yake)). (Hadiyth sahihi: Imetolewa na Abuu Daawuud (383),
na At-Tirmidhiy (143), na Ibnu Maajah (531))
5-
Kuitwaharisha soli ya viatu
Imepokelewa na
Abuu Sa’iyd Allaah Amridhie kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) amesema:
((ﺍﺫﺍ ﺟﺎﺀ ﺃﺣﺪﻛﻢ ﺍﻟﻤﺴﺠﺪ ﻓﻠﻴﻘﻠﺐ ﻧﻌﻠﻴﻪ
ﻭﻟﻴﻨﻈﺮﻓﻴﻬﻤﺎ, ﻓﺎﻥ ﺭﺃﻯ ﺧﺒﺜﺎ ﻓﻠﻴﻤﺴﺤﻪ ﺑﺎﻷﺭﺽ, ﺛﻢ ﻟﻴﺼﻞ ﺑﻬﻤﺎ))
((Anapokuja
mmoja wenu msikitini, basi avigeuze viatu vyake na aangalie vina nini. Ikiwa
ataona najisi, basi aipanguse kwa ardhi, kisha aswali navyo))
(Hadiyth sahihi: Imetolewa na Abuu Daawuud
(646))
6-
Kukitwaharisha chombo mbwa anapokilamba
Imepokelewa
toka kwa Abuu Hurayrah kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) amesema:
((ﻃﻬﻮﺭ ﺍﻧﺎﺀ ﺃﺣﺪﻛﻢ ﺍﺫﺍ ﻭﻟﻎ ﻓﻴﻪ ﺍﻟﻜﻠﺐ ﺃﻥ
ﻳﻐﺴﻠﻪ ﺳﺒﻊ ﻣﺮﺍﺕ ﺃﻭﻻﻫﻦ ﺑﺎﻟﺘﺮﺍﺏ))
((Kukitwaharisha
chombo cha mmoja wenu anapokilamba mbwa ni kukiosha mara saba, moja kati ya
hizo kwa mchanga)) (Hadiyth sahihi: Imetolewa na Muslim (279), na Abuu Daawuud
(71))
7-
Kuitwaharisha ngozi ya nyamafu
Ni kwa kuitia
rangi. Kwa neno lake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((ﺍﺫﺍ ﺩﺑﻎ ﺍﻻﻫﺎﺏ ﻓﻘﺪ ﻃﻬﺮ)
((Inapotiwa
rangi ngozi ya nyamafu, basi imetwaharika)) (Hadiyth sahihi: Imetolewa na
Muslim na mwingine)
8-
Kuitwaharisha ardhi iliyoingia mkojo na mfano wake
Inakuwa ni kwa
kumiminia (maji) juu yake. Kama alivyomrisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) kumwagia maji juu ya mkojo wa bedui msikitini
(Hadiyth sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy
(219), na Muslim (284))
Bila shaka aliamuru hilo kwa ajili ya kuharakia
usafi. Na kama si hivyo, lau kama angeliacha mpaka ukakauka na athari ya najisi
ikaondoka, basi (ardhi) ingetwaharika.
9-
Kukitwaharisha kisima au samli inapoingia ndani yake najis
Inakuwa ni kwa
kuichota na kuiondosha najisi na sehemu za pambizoni mwake, na iliyosalia
inabakia twahara. Ni kwa Hadiyth ya Ibnu ‘Abbaas kwamba Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu panya aliyeangukia katika samli
akasema:
((ﺃﻟﻘﻮﻫﺎ, ﻭﻣﺎ ﺣﻮﻟﻬﺎ ﻓﺎﻃﺮﺣﻮﻩ, ﻭﻛﻠﻮﺍ ﺳﻤﻨﻜﻢ))
((Mtupeni, na
sehemu za pambizoni mwake ziondosheni, na samli yenu kuleni))
(Hadiyth sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy
(Vichinjwa – Mlango wa 34))
Hivi Ndio Namna
Ya kutwaharisha Najisi
Je, Ni Lazima
(kutumia) Maji Katika Kuondosha Najisi? Au Inajuzu Kuondosha Kwa Vimiminika
Vinginevyo Au Mada Nyinginezo?
Maulamaa
wamehitalifiana katika suala hili juu ya kauli mbili mashuhuri:
KAULI YA KWANZA
Ni sharti
kutumia maji kwa ajili ya kuondosha najisi, na wala haisihi kwa kinginecho ila
kwa dalili.
Na hili ndilo
mashuhuri katika madhehebu ya Maalik na Ahmad. Na pia ni madhehebu ya
Ash-Shaafi'iy katika "Al-Jadyd" (rai mpya). Ash-Shawkaany na
waliomfuata, _ ("Bidaayatul Mujtahid" (1/99), na "Al-Ummu"
(1/49), na "As-Saylu Al-Jarraar" (1/49)) ameliunga mkono hili. Na
hoja yao ni:
1- Neno Lake
Ta'aala
((ﻭَﻳُﻨَﺰِّﻝُ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢ ﻣِّﻦ ﺍﻟﺴَّﻤَﺎﺀ
ﻣَﺎﺀ ﻟِّﻴُﻄَﻬِّﺮَﻛُﻢ ﺑِﻪِ))
«Na
Anawateremshieni maji toka mbinguni ili Awatwaharisheni kwayo » (Surat
Al-Anfaal-Aya ya 11)
2- Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru kumwagia maji juu ya
mkojo wa bedui (Imekubaliwa na wote. Na imetangulia hivi punde)
Wamesema kwamba
amri ni ya ulazima, na kwa hivyo haitoshelezi katika kuondosha najisi isipokuwa
kwa maji!!
3- Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kama ilivyo katika Hadiyth ya
Abuu Tha'alabah, aliamuru kukiosha chombo cha Ahlul-Kitaab kwa maji
(Imekubaliwa na wote. Imetolewa na Al-Bukhaariy (5170), na Muslim (1930))
4- Amesema
Ash-Shawkaany: "Maji ndio asili katika kutwaharisha najisi kwa kuelezewa
kwake na Mwekaji sheria kuwa ni twahara yenyewe yenye kutwaharisha kinginecho.
Basi hayaachwi kikatumika kingine ila kama litathibiti hilo toka kwa Mwekaji
sheria. Na kama si hivyo, basi haiwezekani. Kwani hiyo ni kuachana na
kinachojulikana kwamba maji ni twahara kwenda kwenye kisichojulikana kuwa ni
twahara. Na hiyo ni kutoka nje ya vile mikondo ya kisheria inavyokwenda…".
KAULI YA PILI
Inatosheleza
kujitwaharisha kwa kila chenye kuondosha najisi, na si lazima maji.
Na haya ndio
madhehebu ya Abuu Haniyfah, na riwaya nyingine toka kwa Maalik na Ahmad, na
kauli ya zamani ya Ash-Shaafi'iy, na Ibnu Hazm. Nalo ndilo chaguo la Shaykh wa
Uislamu Ibnu Taymiyah, na pia Mwanachuoni Mkubwa Ibnu 'Uthaymiyn
("Al-Badaai'i (1/83), na "Fathul Qadyr" (1/200), na
"Majmu'u Al-Fataawaa" (21/475), na "Al-Muhallaa" (1/92-94),
na "Ash-Sharhu Al-Mumti'i"(1/361-363))
Ni kauli yenye nguvu kwa yafuatayo:
1- Kwamba maji
kuwa ni twahara yenyewe na yenye kutwaharisha kingine, hakuzuii kingine kuwa ni
chenye kutwaharisha vilevile. Kwani kanuni inasema: "Kukosekana sababu
maalumu, hakuhukumii kuondoka kisababisho maalumu, sawasawa ikawa dalili au sio
dalili". Kwa vile chenye kuathiri kinaweza kuwa ni kitu kingine. Na hii
ndio hali halisi kwa upande wa najisi (Ash-Sharhu Al-Mumti'i (1/362))
Ninasema (Abuu
Maalik): "Bali baadhi ya vimiminika kama vile siki na madawa ya kusafishia
ya viwandani, huondosha najisi kama maji au zaidi kuliko maji".
2- Kwamba
Mwekaji sheria Ameamuru kuondosha najisi kwa maji katika masuala maalumu, na
wala Hakuamuru amri jumuishi kwamba kila najisi iondoshwe kwa maji.
3- Kwamba
sheria imeruhusu kuondosha baadhi ya najisi bila maji kama kustanji kwa jiwe,
au kuvisugua viatu kwa mchanga, au kutwaharika nguo inayoburuzika kwa (kugusana
na) ardhi, na mengineyo yaliyotangulia.
4- Kwamba
kuondosha najisi si katika mlango wa kilichoamriwa, bali ni katika mlango wa
kujiepusha na kilichokatazwa. Na ikitokea (ikaondoshwa) kwa sababu yoyote ile,
hukumu itathibiti. Na kwa ajili hiyo, nia haishurutishwi katika kuondosha
najisi. Lakini kama itaondoka kwa kitendo cha mtu aliyenuia, basi atalipwa
thawabu kwa hilo. Na kama si hivyo, kama itaondoshwa bila kitendo chake wala nia
yake, madhara yataondoka, na wala hatokuwa na thawabu wala hatokuwa na
madhambi.
Na hili
linatiliwa nguvu na kwamba pombe inapobadilika na kuwa siki, basi inakuwa
imetwaharika – kwa wale wanaosema kuwa pombe ni najisi – kwa makubaliano ya
Waislamu.
Ninasema (Abuu
Maalik): "Lenye nguvu ni kuwa najisi inapoondoka kwa kitu chochote, hukumu
yake inaondoka na inakuwa ni twahara".
HAPA KUNA FAIDA
KADHAA
1- Faida ya
suala hili ni kuwa mtu ambaye kwenye nguo yake au katika mwili wake kuna
najisi, na akatumia chochote katika madawa twahara ya kusafishia – yasiyo maji
– ili kuondosha najisi hiyo, basi hilo humtosheleza na wala si lazima aoshe kwa
maji.
2- Haijuzu
kutumia vyakula au vinywaji katika kuondoshea najisi bila dharura, kwani huo ni
uharibifu wamali ("Majmu'u Al-Fataawaa" (21/475))
3- Kwamba
utwaharishaji bila maji kwa (kutumia) vimiminika vingine au mada nyinginezo,
bila shaka hufanyika katika (kiini cha) najisi yenyewe inayokuwepo katika nguo
au mwili au mahala. Ama utwaharishaji wa kihukumu (twahara ya hadathi)kama vile
wudhuu, kuoga na mfano wake, haitotosheleza isipokuwa kwa maji.
Na Allaah
Anajua Zaidi
Tunaendelea Na
Somo Letu La Fiqhi
"Je, Damu Inazingatiwa Kuwa Ni Katika
Najisi?"
Damu ina
vigawanyo:
1- DAMU YA
HEDHI:
Damu hii ni
najisi kwa makubaliano ya Maulamaa. Dalili ya unajisi wake tumekwisha isoma
nyuma.
2- DAMU YA
MWANADAMU
(Tafsiri ya Al-Qurtuby (2/ 221), Al-Majmuu
(2/511), Al-Muhalla (1/102), Al-Kaafy (1/110), Bidaayatul Mujtahid, As-Saylul
Jarraar (1/31), Ash-Sharhul Mumti'i (1/376), As-Silsilatu Asw-Swahiyhah na
Tamaamu Al-Minnah (uk.50))
Ni damu
iliyosababisha mahitalifiano juu ya hukumu yake. Lililo mashuhuri kwa watu wa
madhehebu ya kifiqhi ni kwamba damu ni najisi, lakini wao hawana hoja.
Isipokuwa damu imeharamishwa kwa matini ya Qur-aan katika neno Lake
Aliyetukuka:
((ﻗُﻞ ﻻَّ ﺃَﺟِﺪُ ﻓِﻲ ﻣَﺎ ﺃُﻭْﺣِﻲَ ﺇِﻟَﻲَّ
ﻣُﺤَﺮَّﻣًﺎ ﻋَﻠَﻰ ﻃَﺎﻋِﻢٍ ﻳَﻄْﻌَﻤُﻪُ ﺇِﻻَّ ﺃَﻥ ﻳَﻜُﻮﻥَ ﻣَﻴْﺘَﺔً ﺃَﻭْ ﺩَﻣًﺎ
ﻣَّﺴْﻔُﻮﺣًﺎ ﺃَﻭْ ﻟَﺤْﻢَ ﺧِﻨﺰِﻳﺮٍ ﻓَﺈِﻧَّﻪُ ﺭِﺟْﺲٌ ))
« Sema: Sioni
katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila
isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayomwagika, au nyama ya nguruwe, kwani
hiyo ni uchafu» (Surat Al-An ‘aam: 145)
Kwa hiyo, wao
wamewajibisha unajisi wake kutokana na kuharamishwa kwake,kama walivyofanya
katika pombe, na wala hayafichikani yaliyomo ndani yake. Lakini amenukuu zaidi
ya Mwa- nachuoni mmoja katika Maulamaa kuwa wanakubaliana wote (ijmaa) juu ya
unajisi wake. Maelezo zaidi yatakuja katika hilo.
Ni wakati
ambapo kundi la waliokuja baadaye akiwemo Ash-Shawkaany, Siddiyq Khaan,
Al-Albaaniy, Ibnu ‛Uthaymiyn (Allaah Awarehemu) wameelekea kusema kuwa damu ni
twahara kwa kutothibiti ijmaa kwa upande wao. Wao wametoa dalili vilevile kwa
haya yafuatayo:
1-
Asili ya vitu ni twahara mpaka iwepo
dalili kuwa ni najisi. Na sisi "hatujui" kwamba Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru kuosha damu nyingine isiyo ya hedhi
ingawa mtu hupatwa mara nyingi na majeraha na mfano wake. Na lau kama damu ni
najisi, basi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) angelibainisha,
kwa sababu hali ya mambo inahitajia hilo.
2-
2- Ni kwamba Waislamu bado wanaswali
wakiwa na majeraha yao, na wanaweza kuchuruzikwa na damu nyingi ambayo si ya
kusamehewa. Na wala haikupokelewa toka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) kwamba aliamuru kuiosha, na wala haikupokelewa kwamba wao
walikuwa wakijilinda nayo kwa hadhari kubwa.
3-
- Amesema Al-Hasan: "Waislamu
bado wanaswali wakiwa na majeraha yao".
4-
(Isnadi yake ni sahihi. Imepokelewa na
Al-Bukhaariy ikiwa "muallaq" (1/336). Na Ibnu Abu Shaybah
ameiunganisha kwa sanad sahihi kamailivyo katika Al-Fath (1/337))
5-
6-
7-
Na katika kisa cha Swahaba Muanswaar
aliyekuwa amesimama usiku akiswali. Mshirikina alimpiga mshale, akauweka, kisha
akaunyofoa, mpaka akampiga mishale mitatu. Kisha alirukuu, akasujudu na
akaendelea na Swalah yake na huku akivuja damu.
8-
( Hadiyth Sahihi: Al-Bukhaariy ameifanya
"mu’allaq" (1/336), na Ahmad na wengineo wameiunganisha, nayo ni
sahihi)
9-
10- -
Al-Albaaniy(Allaah Amrehemu)
11- (Tamaam Al-Minnah (51,52))
12- amesema:
"Nayo iko katika hukumu ya Hadiyth Marfuu, kwa vile kwa kawaida
haiyumkiniki kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) asilijue
hilo. Na lau kama damu nyingi ingelikuwa ni yenye kuvunja (kubatilisha Swalah),
basi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) angelibainisha, kwani
kuchelewesha kubainisha (jambo) wakati ule wa kuhitajika, haifai kama
inavyojulikana katika taaluma ya "usuul". Na kama tutachukulia kwamba
hilo lilifichikana kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi
halifichikani kwa Mwenyezi Mungu Ambaye hakifichikani Kwake chenye kujificha
sawasawa ardhini au mbinguni. Na lau kama (damu) ingelikuwa ni yenye
kubatilisha au ni najisi, basi lingefunuliwa hilo kwa Mtume kama ilivyo wazi,
haifichikani kwa yeyote…..".
13-
14- - Na
katika kisa cha kuuawa ‘Umar bin Al-Khatw-twaab (Allaah Amridhie): "Umar
aliswali, na huku jeraha lake linachuruzisha damu". (Hadiyth Sahihi:
Imetolewa na Maalik (82), na amepokea toka kwake Al-Bayhaqiy (1/357) na
wengineo kwa sanad sahihi)
15-
16-
17- 3-
Ni kwa Hadiyth ya 'Aaishah katika kisa cha kufa kwa Sa'ad bin Mu’adh. Alisema:
"Wakati Sa'ad bin Mu’adh alipojeruhiwa siku ya Khandaq, mtu mmoja alimpiga
mshale wa kwenye mshipa wa damu mkononi. Mtume alimpigia hema msikitini ili
amtazame kwa karibu. Na akiwa katika hali hiyo, usiku mmoja ghafla jeraha lake
lilipasuka na damu ikachuruzika toka katika kidonda chake. Wakasema: Enyi watu
wa nyumba! Nini hiki kinatujia toka kwenu? Wakatazama. Na kumbe Sa'ad jeraha
lake limepasukana damu ikifoka, akafariki
18- (Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Abuu Daawuud
(3100) kwa ufupi, na At-Twabaraaniy katika (Al-Kabiyr) (6/7))
19-
20-
21- Kauli
ya Mwandishi Wa Fiqhi:
22-
23- Ninasema
(Abuu Maalik): "Na wala haikupokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) aliamuru maji yamwagiwe juu yake na hasa kwa vile yuko
msikitini kama alivyoamuru kumwagia maji juu ya mkojo wa bedui.
24- 4-
Kwamba Ibnu Rushdi wakati alipotaja hitilafu za Maulamaa kwa upande wa damu ya
samaki, alieleza kwamba sababu ya kuhitalifiana kwao, ni kuhitilafiana kwao
katika maiti yake. Basi mwenye kuifanya maiti yake inaingia chini ya ujumuishi
wa kuharamishwa, ataifanya damu yake hivyo hivyo. Na mwenye kuitoa maiti yake,
ataitoa damu yake kwa kupimia maiti yake.
25- Na
tunasema: "Wao wanasema kuwa maiti ya mwanadamu ni twahara, na kwa hivyo
damu yake vilevile (ni twahara) kwa mujibu wa kanuni yao".
26- Na
kwa ajili hiyo, Ibnu Rushdi alisema baada yake: "Na matini bila shaka
imeonyesha juu ya unajisi wa damu ya hedhi, na isiyokuwa hiyo, basi iko katika
uasili uliokubaliwa na wenye kuzozana, nayo ni twahara. Na haitoki humo ila kwa
matini ya kusimamishia hoja…".
27-
28- Na
ikiwa itasemwa: "Je, haipimiwi kwa damu ya hedhi, na damu ya hedhi ni
najisi?
29- Tunasema:
"Hiki ni kipimo pamoja na tofauti:
30- -
Kwani damu ya hedhi ni damu ya maumbile ya asili kwa wanawake. Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
31-
32-
((ﺍﻥ ﻫﺬﺍ ﺷﻴﺊ ﻛﺘﺒﻪ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻰ ﺑﻨﺎﺕ ﺁﺩﻡ))
33-
34- ((Hakika
hiki ni kitu ambacho Mwenyezi Mungu Amekiweka kwa mabinti wa Aadam (wanawake))
35- (Hadiyth Sahihi: Al-Bukhaariy (294), na Muslim
(1211))
36-
37- Na akasema katika istihaadha:
38-
39- ((ﺍﻧﻪ ﺩﻡ ﻋﺮﻕ))
40-
41- ((Hakika
hiyo ni damu ya mshipa (asili)) (Hadiyth Sahihi: Al-Bukhaariy (327), na Muslim
(333))
42- Kisha
hakika damu ya hedhi ni damu nzito iliyovunda na yenye harufu mbaya. Imefanana
na mkojo na kinyesi, si damu yenye kutoka katika zisizo njia mbili